KIUNGO
Arturo Vidal anayetakiwa na Manchester United ameonyesha ishara fulani,
baada ya kusaini jezi ya shabiki wa Mashetani hao Wekundu akiwa kwenye
ziara na klabu yake, Juventus nchini Australia.
Vidal,
ambaye amekuwa akihusishwa na kuhamia Old Trafford kwa muda sasa baada
ya nyota huyo wa Chilea kung'ara msimu uliopita, amekuwa akishawishiwa
na wachezaji wenzake kubaki Italia.
Kiungo
mwingine wa Juventus, Paul Pogba alisema wiki iliyopita kwamba
anatumaini Vidal atabakia katika klabu hiyo, licha ya kutakiwa na
United, lakini hali inaonekana kuwa tofauti baada ya kusaini jezi ya
United.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni