VERSE 1:
Ulianza wewe.. wakaja waimbaji na wabana pua/
Wale mwewe.. Franga wawindaji wakatusua/
Kwakuwa.. wanajua mshikaji unaishi kwa miko/na zako itikadi.. ziko kimziki na sio mshiko/
Kama haileti hela..basi haimake sense.. no sweat kisela mie nikakomaa tu na lako penzi/
Sikusound garbage au kuchange suddenly../
Mie ni mjeshi so naweza fight savagely/
Hiphop ya ukweli.. ukapigwa radioni/sometimes malaika wa heri nao hutembelea motoni/
Penzi ni kipofu na anayemuona halioni/ sikuwa na hofu.. mama alinipenda tangu nikiwa tumboni/
I started young.. I made my mother's womb a drum/
My umblirical chord a guitar.. muhoji aliyenizaa/
BONGOFLAVA mzuri kiasi.. hiphop we ndo my queen/ my 1st.. my last & everything in betweenjj
Chorus:
Mimi na wewe.. tangu long time/ Kabla ya hizi pesa kabla haijaja hii Fame/
Cha ajabu haujabadilika na upo kwenye mainstream… BONGO HIPHOP X2
'
VERSE 2:
Kama kukupenda wewe ni dhambi.. basi shetani yu nami/ na kamwe sintonyea kambi ili niwabambe dukani/
For a million little pieces naweza kumcon Oprah ka James Frey/
Na watasema sitishi wakati wanaogopa nisitokee/
Waufuate mkumbo huu wa wasomi.. wa midundo na mistari/ ukiwa na nyundo mkononi.. ni rahisi kupigilia msumari/
Sio tu bongo.. mpaka Ng'ambo hakuna uhuru wa habari/ kuna uhuru wa mwenye chombo.. mitambo na mwenye mali/
Kujifanya hawasikii.. haiwasaidii.. wala haiwajengi/ unachosema ni.. kamwe IPP haitompinga Mengi/
Unawakumbusha wazazi wa uswazi.. chati ya uteja imeingia/ na Mapusha wanauza drugs ili walishe familia/
Mbaya.. kuhifadhi fuvu la mtu ndani ya kabati/ mbaya zaidi ni kuwa na ndugu.. halafu kichwa maji/
Amka bongo lala.. hiphop sio ufala.. ni lazima uifate/
Uaminifu ni kama mshahara.. fanya kazi ili uupate
Chorus:
Mimi na wewe.. tangu long time/ Kabla ya hizi pesa kabla haijaja hii Fame
Cha ajabu haujabadilika na upo kwenye mainstream… BONGO HIPHOP X2
VERSE 3:
Mapenzi ya sikuhizi.. bila kugombana yanakua hayana stimu/
Pia ni ruksa kushikana lakini sio kushikiana simu/
Inanipa wazimu.. kusikia kimwana haujaachana na Hasheem/
Na bado mnawasiliana..una mpango wa kuchanganya timu?/
Nakupenda hiphop.. ndo maana ninarap ile mbaya/
Naspit fire bila hennessy.. au kula kaya/
I want my art to be my legacy.. kabla sijaretire.. waanze nigwaya hawa enemies.. anyways NI HAYO TU/
Beef huletwa na wivu.. na wivu sio hiphop/
Chorus:
Mimi na wewe.. tangu long time/ Kabla ya hizi pesa kabla haijaja hii Fame/
Cha ajabu haujabadilika na upo kwenye mainstream… BONGO HIPHOP X2
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni