Mshambuliaji wa England, Wayne Rooney akishangilia baada ya kufunga bao dhidi ya Uruguay katika fainali ya kombe la dunia.
"Sitasahau siku Roy Hodgson aliponifanya
nipae futi 10 juu. Ilikuwa katikati ya wiki mchana nikipumzika nyumbani
baada ya mazoezi. Roy alinipigia simu na kuniambia: nina habari muhimu:
Nilikuwa naenda kuwa nahodha wa England".
"Sikuweza kuamini kabisa na ninaamini
hali kama hiyo itajitokeza kwa Wayne Rooney wiki hii ambapo mrithi wangu
atatajwa. Kwa vile nami nahusika, ndiye mtu anayestahili kwa sasa".
Roy ana imani kubwa na Wayne. Wakati
Manchester United ikiwa katika presha msimu uliopita, wakati ule kuna
tetesi nyingi kuhusu nafasi yake katika timu ya taifa, bado kocha wake
alimpanga katika michezo muhimu. Ilikuwa nzuri na heshima kubwa kwake.
Wakipunga upepo: Rooney (kushoto) na Steven Gerrard wakipumzika baada ya kumaliza programu ya mazoezi mjini Algarve mwezi mei.
Nahodha: Rooney (kulia) aliiongoza
Manchester United katika mechi ya kirafiki ya maandalizi ya msimu dhidi
ya Valencia Agosti 12 mwaka huu.
Mashetani wekundu: Rooney akishangilia
baada ya kufunga bao dhidi ya Swansea kwenye mechi ya ufunguzi ya ligi
kuu soka nchini England.
Labda makocha wengi wanaweza kumuondoa
katika kikosi cha kwanza na kumuweka benchi, lakini Roy anajua kuwa
Wayne bado ana mchango mkubwa katika kikosi chake na ataendelea
kuchangia kwa miaka michache ijayo.
Kwanini nadhani Wayne ndiye chaguo la
kwanza?, Kiasili ni kiongozi. Mbali na kuwa mchezaji wa kiwango cha juu,
ana uwezo wa kutengeneza heshima katika kikosi, Wayne ana mapenzi ya
kuliwakilisha taifa lake na hataogopa majukumu hayo.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni