Mshambuliaji wa Atletico Madrid,
Mario Mandzukic akifunga bao la kuongoza dhidi ya Real Madrid katika
mchezo wa marudiano wa 'Spanish Super Cup'
REAL Madrid wameanza vibaya msimu mpya
baada ya jana kupigwa bao 1-0 na mahasimu wao Atletico Madrid katika
uwanja wa Vicente Calderon na kupoteza kombe la 'Spanish Super Cup'.
Mechi ya kwanza Santiago Bernabeu timu hizo zilitoka sare ya 1-1, hivyo Atletico kushinda kwa wastani wa mabao 2-1.
Bao pekee la ushindi wa Atletico
lilitiwa kambani na mshambuliaji mpya ambaye unaweza kusema amerithi
mikoba ya Diego Costa, Mario Mandzukic.
Msimu uliopita, kikosi cha Diego Simeone
kiliwazidi kete Real Madrid na kutwaa kombe la ligi kuu maarufu kama La
Liga, sasa wamewashinda katika kombe la 'Spanish Super Cup'
Real Madrid wametumia fedha nyingi
kununua wachezaji nyota katika kombe la dunia lililopita, lakini jambo
la kuwaunganisha na kuwafanya wacheze kitimu ni muhimu zaidi.
Carlo Ancelotti ana kazi kubwa zaidi
kwasababu jana walijikuta wakiwa nyuma kwa bao 1-0 katika sekunde ya 80
(sawa na dakika 2) na walishindwa kutafuta upenyo wa kusawazisha.
Kikosi
cha Atletico Madrid: Moya; Juanfran, Godín, Miranda, Siqueira; Tiago,
Gabi; Koke, Raul García, Griezmann (Jiminez 73); Mandzukic
Wachezaji wa akiba: Oblak, Suarez, Rodriguez, Ansaldi, Niguez, Gimenez
Kikosi
cha Real Madrid: Casillas; Carvajal, Varane, Ramos, Coentrao (Marcelo
70); Modric, Kroos (Ronaldo 45), Xabi Alonso; James (Isco 65), Benzema,
Bale
Wachezaji wa akiba: Navas, Pepe, Arbeloa, Illarra
Shujaa wa goli: Mshambuliaji wa Atletico, Mario Mandzukic akinyanyua kombe la Super Cup baada ya kuifunga Real Madrid jana
Mabingwa: Atletico wameanza msimu kwa kuwazidi kete mahasimu wao na kutwaaa kombe
Shangwe: Nyota wa Atletico, Mario
Mandzukic (katikati) akishangalia bao lake la sekunde ya pili dhidi ya
Real Madrid katika dimba la Vicente Calderon
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni