STAY WITH US

LightBlog

Breaking

TANGAZA NASI: +255 655 442 255

TANGAZA NASI: +255 655 442 255

CHANZI OPEN SCHOOL

CHANZI OPEN SCHOOL

Alhamisi, 25 Septemba 2014

GYAN AKANA KUMTOA KAFARA RAFIKI YAKE.


MSHAMBULIAJI nyota wa kimataifa wa Ghana, Asamoah Gyan ametoa taarifa kukanusha kuhusika na kifo cha mwanamuziki wa rap nchini Ghana Castro. Castro ambaye ni rafiki wa mshambuliaji huyo wa zamani wa klabu ya Sunderland alipotea katika mazingira ya kutatanisha sambamba na rafiki yake wa kike Janet Bandu Julai mwaka huu. Mwanamuziki huyo ambaye jina lake halisi ni Theophilus Tagoe na mpenzi wake walitoweka baharini wakati wakiwa likizo na familia ya Gyan jijini Ada. Kumekuwa na taarifa za kuhusishwa na mambo ya kimazingara kwa kupotea kwa Castro jambo ambalo limepingwa na Gyan kwa kukataa kuhusika na lolote. Miili ya wawili hao haikuwahi kupatikana na madai yaliendelea kusambazwa mwezi huu wakati ambapo kakake Gyan, Baffour Gyan alidaiwa kuwa mmoja wa genge la vijana waliowashambulia wandishi wa habari waliohoji maswali kuhusu madai hayo. Wakili wake Kissi Agbyabeng alitoa taarifa akisema kuwa familia ya Gyan imeshangazwa sana na madai hayo na iliamua kutosema chochote ili polisi waendelee na uchunguzi wao.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

KAMATI YA TUZO IMEFANYA MCHUJO KWENYE WACHEZAJI 30 WAMEBAKI 15, MKUDE, AJIBU WAMETOLEWA, ANGALIA ORODHA

Kamati ya Tuzo za Ligi Kuu ya Vodacom (VPL), iliyokutana wiki hii imeteua wachezaji 15 kwa ajili ya kuwania Tuzo ya Mchezaji Bora wa VPL msi...

TIBA YA KIIMANI

TIBA YA KIIMANI

a

a
Adbox