KIUNGO wa Chelsea,
N’Golo Kante ametuliwa kuwa mchezaji bora wa mwaka na Chama cha
Waandishi wa Habari za Soka.
Nyota huyo mwenye umri wa miaka 26
ameisaidia Chelsea kuongoza msimamo wa Ligi Kuu huku pia akiisaidia
Leicester City kutwaa taji lao la kwanza la ligi msimu uliopita.
Mapema
mwezi uliopita Kante aliteuliwa kutwaa tuzo ya mchezaji bora wa mwaka wa
Chama cha Wachezaji Bora wa Kulipwa-PFA huku pia akitajwa kwenye kikosi
bora cha PFA kwa mwaka wa pili mfululizo.
Nyota huyo wa kimataifa wa
Ufaransa amecheza mechi 33 za ligi akiwa na Chelsea msimu huu, huku
akifunga bao moja na kusaidia lingine moja lakini msaada wake anaotoa
kwenye safu ya ulinzi ndio uliomtengenezea sifa kubwa.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni