
Kwa mujibu wa mitandao ya Misri, Youm7 na Yallakora inasemekana Bodi ya Zamalek imeridhika na uwezo wa Msuva baada ya kumtazama katika siku za hivi karibuni,
Tayari bodi hio imeamua kutuma wawakilishi wake kuja nchini Tanzania kuzungumza na Msuva pamoja na Yanga viongozi wa Yanga.
Msuva ambaye mabao 19 msimu huu ana mkataba wa miaka mitatu na Yanga ambao unatazamiwa kuisha mwezi Mei mwakani.
Mchambuzi wa Soka la Uarabuni, Lotfi Wada amesema Msuva ni chaguo zuri kwa Zamalek wanaotafuta mshambuliaji mzuri lakini kutokana na kuyumba kwa uchumi wa nchi na kupanda kwa dola klabu nyingi za Misri zinalazimika kutazama wachezaji wa bei nafuu kinyume na ilivyozoeleka.
Chanzo: soka360
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni