Mara baada ya michezo ya mwishoni mwa juma lililopita, Ligi Kuu ya
Vodacom Tanzania Bara 2016/2017, inatarajiwa kuendelea Jumanne Mei 9,
mwaka huu kwa mchezo mmoja ambako Mabingwa watetezi wa Kombe hilo, Young
Africans itaikaribisha Kagera Sugar y Kagera katika mchezo
utakaofanyika Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam kuanzia saa 10.00 jioni.
Kwa mujibu wa ratiba ya Ligi Kuu ya Vodacom, mechi nyingine mbili
zitachezwa Ijumaa Mei 12, 2017 ambako Simba SC itaialika Stand United FC
ya Shinyanga kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam wakati Azam FC siku
hiyo hiyo ya Mei 12, mwaka huu itakuwa mwenyeji wa Toto Africans ya
Mwanza kwenye Uwanja wa Azam ulioko Chamazi, Dar es Salaam.
Jumamosi Mei 13, mwaka huu JKT Ruvu itakuwa nyumbani Uwanja wa
Mkwakwani jijini Tanga kucheza na Majimaji ya Songea wakati Tanzania
Prisons itaikaribisha Ndanda ya Mtwara kwenye Uwanja wa Sokoine jijini
Mbeya ilihali Mwadui ya Shinyanga itakuwa mgeni wa Mtibwa Sugar Uwanja
wa Manungu ulioko Mvomero, Morogoro huku Mbeya City ikisafiri hadi Dar
es Salaam kucheza na Young Africans kwenye Uwanja wa Uhuru, Dar es
Salaam.
Siku ya Jumapili Mei 14, mwaka huu African Lyon ya Dar es Salaam
itacheza na Ruvu Shooting kwenye Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam ilihali
siku inayofuata, Jumanne Mei 16, mwaka huu Young Africans tena itakuwa
mwenyeji wa Toto Africans kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Funga dimba la Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara itakuwa Mei 20,
mwaka huu kwa timu zote kucheza ambako Azam FC itakuwa mwenyeji wa
Kagera Sugar kwenye Uwanja wa Chamazi, Dar es Salaam wakati Majimaji
itamaliza na Mbeya City kwenye Uwanja wa Majimaji mjini Songea wakati
Simba na Mwadui zitacheza Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Siku hiyo Mbao FC itaialika Young Africans ya Dar es Salaam kwenye
Uwanja wa CCM Kirumba, Mwanza wakati Stand United itamaliza na Ruvu
Shooting ya Pwani kwenye Uwanja Kambarage mjini Shinyanga ilihali Mtibwa
Sugar itakuwa mwenyeji wa Toto Africans ya Mwanza kwenye Uwanja wa
Manungu, Morogoro wakati Africans Lyon ikiwa mgeni wa Tanzania Prisons
kwenye Uwanja wa Sokoine jijini Mbeya na Ndanda itamaliza na JKT Ruvu
mjini Mtwara kwenye Uwanja wa Nangwanda Sijaona
TANGAZA NASI: +255 655 442 255
CHANZI OPEN SCHOOL
Jumatatu, 8 Mei 2017
HIZI HAPA MECHI ZOTE ZILIZO BAKI KWENYE VPL KWA TIMU ZOTE
About asantemuya
Soratemplates is a blogger resources site is a provider of high quality blogger template with premium looking layout and robust design. The main mission of templatesyard is to provide the best quality blogger templates.
Jisajili kwenye:
Chapisha Maoni (Atom)
KAMATI YA TUZO IMEFANYA MCHUJO KWENYE WACHEZAJI 30 WAMEBAKI 15, MKUDE, AJIBU WAMETOLEWA, ANGALIA ORODHA
Kamati ya Tuzo za Ligi Kuu ya Vodacom (VPL), iliyokutana wiki hii imeteua wachezaji 15 kwa ajili ya kuwania Tuzo ya Mchezaji Bora wa VPL msi...
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni