STAY WITH US

LightBlog

Breaking

TANGAZA NASI: +255 655 442 255

TANGAZA NASI: +255 655 442 255

CHANZI OPEN SCHOOL

CHANZI OPEN SCHOOL

Ijumaa, 28 Novemba 2014

PIGO ARSENAL, WILSHERE NJE MIEZI MINNE BAADA YA 'KUPIGWA KISU' JANA

KLABU ya Arsenal inakabiliwa na baa la majeruhi, baada ya Jack Wilshere naye kutakiwa kuwa nje kwa miezi minne kufuatia kufanyiwa upasuaji wa kifundo cha mguu jana.
Na kocha Arsene Wenger atalazimika kuingia sokoni Januari kununua wachezaji ili kupoza maumivu ya tatizo la majeruhi kikosini mwake. 
Wilshere amefanyiwa upasuaji wa kifundo cha mguu wake wa kushoto baada ya kipigo cha Manchester United cha mabao 2-1 Uwanja wa Emirates Jumamosi iliyopita. Na Nahodha, Mikel Arteta
pia
anaweza asicheze tena mwaka huu baada ya kuumia Arsenal ikishinda 2-0 dhidi ya Borussia Dortmund.
Wilshere posted a picture of his ankle in a cast after the operation and insisted he will return soon
Wilshere ameposti picha hii baada ya kufanyiwa upasuaji

Kuuminia kwa Wilshere kunamfanya kocha Arsene Wenger awakose viungo wote watatu tegemeo, Aaron Ramsey, Mathieu Flamini na Tomas Rosicky.
Baada ya upasuaji huo, Wilshere akaposti picha Instagram akiwaambia mashabiki wa timu hiyo kwamba zoezi limekwenda vizuri.
"Kifundo cha mwishowe kilihitaji upasuaji," ameandika. "Zoezi limekwenda vizuri na asante kwa mkuu James Calder (mpasuaji)!
Wilshere was clearly in pain after the tackle and it is unlikely that he will be back for Arsenal before March
Wilshere akiugulia maumivu baada ya kuumia na anatarajiwa kurejea kikosini Arsenal kabla ya Machi, mwakani

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

KAMATI YA TUZO IMEFANYA MCHUJO KWENYE WACHEZAJI 30 WAMEBAKI 15, MKUDE, AJIBU WAMETOLEWA, ANGALIA ORODHA

Kamati ya Tuzo za Ligi Kuu ya Vodacom (VPL), iliyokutana wiki hii imeteua wachezaji 15 kwa ajili ya kuwania Tuzo ya Mchezaji Bora wa VPL msi...

TIBA YA KIIMANI

TIBA YA KIIMANI

a

a
Adbox