Nyota
wa Chelsea Eden Hazard alishindwa kuhudhuria sherehe ambapo alitakiwa
kutunukiwa tuzo ya mchezaji bora msimu kwa waandishi wa habari baada ya
kuwa akiuguza majeraha yake yaliyotokana na upasuaji wa fizi aliofanyiwa
hivi karibuni.
Hazard
ambaye alijinyakulia kura za kutosha kutoka kwa waandishi, huku akipata
asilimia 53 na kumzidi Harry Kane wa Tottenham ambaye alishika nafasi
ya pili, alitakiwa kukabidhiwa zawadi yake katika sherehe zilizofanyika
jijini London.
"Shukrani za dhati ziwafikie Waandishi wa Habari za Michezo nchini Uingereza kwa kunichagua kuwa mchezaji wao wa msimu. Naomba radhi kuwa sitaweza kuhudhuria usiku huu mahala hapo lakini tafadhali mnatakiwa kufahamu kuwa ninajivunia sana juu ya hii zawadi ambayo kwangu mimi ni kubwa sana," aliandika hivyo kwenye ukurasa wake wa Twitter.

Hakuna maoni:
Chapisha Maoni