Taarifa zilianza kuzagaa baada ya nyota huyo wa zamani wa Chelsea mwenye umri wa miaka 28, kuandika katika ukurasa wake wa mtandao wa kijamii kuwa anataka kusubiri mpaka wakati wa ndoa kabla ya kukutana kimwili na mpenzi wake.
Akihojiwa Luiz amesema watu wanasema mambo ambayo hawayafamu kwani sio kweli kwamba hajawahi kukutana kimwili na mwanamke. Beki huyo aliendelea kudai kuwa tayari ameshakuwa na wapenzi zaidi ya mmoja katika maisha yake hivyo watu wanapaswa kuheshimu maisha binafsi ya mtu
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni