Manchester United jana usiku wamethibitisha kumsajili Golikipa wa Argentina ambaye ni mchezaji huru, Sergio Romero.
Romero mwenye miaka 28 amesaini mkataba wa miaka mitatu kuitumikia miamba hiyo ya Old Trafford.
Kipa huyo ametua Man United kurithi mikoba ya Victor Valdes ambaye anaondoka majira haya ya kiangazi.
Romero alikuwa sehemu ya kikosi cha AZ Alkmaar kilichobeba ubingwa wa ligi ya Uholanzi mwaka 2009 chini ya Louis van Gaal.
Mlinda mlango huyo amejiunga na wachezaji wenzake wa United waliopo Marekani kujiandaa na msimu mpya.
Baada ya kusaini mkataba, Romero amesema:
'Kiukweli nimefurahi kujiunga na Manchester United. Kucheza timu kubwa duniani ni ndoto iliyotimia".
"Louis van Gaal ni kocha wa ajabu, siwezi kusubiri kuanza maisha mapya tena, napenda changamoto katika maisha yangu ya soka"
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni