STAY WITH US

LightBlog

Breaking

TANGAZA NASI: +255 655 442 255

TANGAZA NASI: +255 655 442 255

CHANZI OPEN SCHOOL

CHANZI OPEN SCHOOL

Jumapili, 26 Julai 2015

SIMBA SC KUCHEZA MECHI YA KWANZA CHINI YA KERR KESHO

SIMBA SC kesho inatarajiwa kucheza mchezo wa kwanza chini ya kocha mpya, Muingereza Dylau Kerr itakapomenyana na Kombaini ya Zanzibar Uwanja wa Amaan, visiwani humo.

Wachezaji wa Simba leo wamepewa mapumziko ya siku moja kwa ajili ya kuupumzisha miili kabla ya kesho Saa 2:00 asubuhi kufanya mazoezi ya viungo tayari kwa kuikabili timu ya Zanzibar Saa 11:00 jioni.

Kocha Mkuu wa Simba SC, Dylan Kerr amesema mechi ya kesho itakuwa ni kipimo kizuri kwa timu yake kujitayarisha na mechi dhidi ya AFC Leopards ya Kenya katika kilele cha tamasha la Simba Day. 

"Tunategemea kufanya vizuri katika mchezo wa kesho na si kesho tu bali hata kwenye mechi yetu kubwa ya kwanza na AFC Leopards,”amesema Muingereza huyo.

Simba itaikabili AFC Leopards Agosti 8, mwaka huu Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

Siku hiyo, wanachama wote wa Simba wenye kadi mpya wataingia bure uwanjani.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

KAMATI YA TUZO IMEFANYA MCHUJO KWENYE WACHEZAJI 30 WAMEBAKI 15, MKUDE, AJIBU WAMETOLEWA, ANGALIA ORODHA

Kamati ya Tuzo za Ligi Kuu ya Vodacom (VPL), iliyokutana wiki hii imeteua wachezaji 15 kwa ajili ya kuwania Tuzo ya Mchezaji Bora wa VPL msi...

TIBA YA KIIMANI

TIBA YA KIIMANI

a

a
Adbox