Wakiwa
tayari wameshinda kombe la pili la FA mfululizo msimu uliopita, Arsenal
jana wametwaa kombe la pili katika mechi za maandalizi ya msimu mpya
wakiichapa 1-0 Wolfsburg na kunyanyua kombe la Emirates.
Mapema mwezi huu, Arsenal walishinda taji la Barclays Asia Trophy nchini Singapore.
Bao pekee la Theo Walcott lilitosha kuipa ushindi Arsenal na sasa wameelekeza nguvu kwenye mechi yao ya ngao ya Hisani dhidi ya Chelsea itayopigwa Wikiendi ijayo dhidi ya Chelsea.
Baada ya ubingwa hao, baadhi ya nyota wa Arsenal wali-tweet hivi...
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni