Wawakirishi wa Tanzania Bara katika michuano ya Klabu bingwa Afrika pamoja na Kombe la Shirikisho, Azam FC pamoja na Yanga zitalazimika kujilipia Hotel pindi watakapokuwa wakienda nje ya Nchi kucheza na wapinzani wao.
Hari hiyo imekuja kufatia Shirikisho la Mpira wa miguu Afrika CAF, kufanyia
marekebisho kanuni zake za michuano ya ngazi ya klabu kwa upande wa malazi ambapo sasa timu zitachagua na kujilipia zenyewe hoteli zinapokuwa kwenye mechi za ugenini.
Kabla ya marekebisho ya kanuni hiyo, timu ngeni ilikuwa ikilipiwa hoteli na timu mwenyeji kwa msafara usiozidi watu 25. CAF ilikuwa imepitisha hoteli maalumu katika kila nchi ambapo mwenyeji alitakiwa kuziweka timu ngeni.
Kwa marekebisho hayo, Chama cha Mpira wa Miguu cha nchi mwenyeji kitakuwa na wajibu wa kuitafutia hoteli timu ngeni iwapo tu kitaombwa kufanya hivyo, lakini jukumu la kulipia malazi litakuwa la timu yenyewe.
Azam inacheza Ligi ya Mabingwa (CL) ambapo itaanzia nyumbani Februari 15 mwaka huu kwa kuikaribisha El Merreikh ya Sudan kwenye Uwanja wa Azam Complex jijini Dar es Salaam.
Nayo Yanga itacheza michuano ya Kombe la Shirikisho (CC), na imepangiwa kucheza mechi ya kwanza nyumbani dhidi ya BDF IX ya Botswana. Mechi hiyo itafanyika Februari 14 mwaka huu Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni