STAY WITH US

LightBlog

Breaking

TANGAZA NASI: +255 655 442 255

TANGAZA NASI: +255 655 442 255

CHANZI OPEN SCHOOL

CHANZI OPEN SCHOOL

Jumatatu, 12 Septemba 2016

BREAKING NEWS; MICHO KAFUNGUKA JUU YA MPANGO WAKE WA KUIFUNDISHA STARS.........


 Tokeo la picha la BREAKING NEWS


” Wachezaji wa Tanzania ni wazuri sana lakini wanahitaji kubadilishwa kutoka kwenye soka la kufurahisha jukwaa na kwenda katika ushindani. ”

image

” Wakati wa michuano ya Cecafa mwaka jana niliwatazama na kubaini walikuwa bora zaidi ya timu zote lakini hawakuwa wanacheza soka la ushindani, zaidi walikuwa wamejikita zaidi katika soka la kufurahisha jukwaa. ”

Hayo ni maneno ya kocha wa timu ya Taifa ya Uganda, Milutin ‘Micho’ Sredojevic akielezea kwa nini hawezi kuogopa kuchukua kibarua cha kuinoa Taifa Stars na kuipeleka AFCON.

Tokeo la picha la taifa stars


Katika mahojiano  Micho ameweka wazi kuwa yupo tayari kuchukua mikoba ya Charles Boniface Mkwasa ambaye anatarajia kumaliza mkataba wake mwezi Februari mwakani.

” Kama Watanzania watanihitaji nitayatathimini kwa undani mapendekezo na ombi lao kwani huwa naangalia mpango ulio bora zaidi.”

Micho aliyewahi kuinoa Yanga ameshangazwa na madai ya Tanzania kuwa na changamoto ya wachezaji wanaoweza kuipeleka AFCON na kudai si kweli.

” Changamoto ipi waliyonayo wachezaji wa Tanzania zaidi ya kubadilika kutoka katika soka la maonesho na kuingia katika soka la kusaka matokeo uwanjani. ”

Amesisitiza kuwa hawezi kuongelea kwa nini msururu mrefu wa makocha wa zamani wa Taifa Stars walishindwa kuipeleka Tanzania katika madhindano ya AFCON lakini binafsi anaamini ndoto hio inawezekana.


” Siwezi kuwasemea makocha wengine lakini binafsi naamini nawafahamu vizuri wachezaji wa Tanzania. Nafahamu uimara na udhaifu wao.

Amemalizia kwa kusema kuwa kwa sasa anabakia kuwa kocha wa Uganda na anaheshimu na kuwajibikia mkataba wake.

Wiki iliyopita mara baada ya kuipa Uganda tiketi ya AFCON Micho aliwashtua wengi kwa kuweka wazi kuwa amefanya kazi bila kulipwa mishahara yake kwa miezi kadhaa na shirikisho la Mpira la Uganda.

Wakati huo
 
Juuko_1

Kocha wa timu ya taifa ya Uganda, Milutin ‘Micho’ Sredojevic amezungumzia mjadala wa beki wake tegemeo, Juuko Murshid kupigwa benchi katika klabu ya Simba.

Micho aliyeipeleka Uganda kwenye michuano ya AFCON kwa mara ya kwanza baada ya miaka 38 amerusha kijembe kwa makocha wa Simba kwa kudai Soka la Tanzania litapiga hatua kwa kutumia aina ya wataalam wenye maamuzi ya kumweka benchi Juuko.

Akizungumza  kujibu madai ya Juuko kutoendana na mfum wa Simba, Micho amesema,

” Tanzania itafika mbali sana kwa aina ya hawa wataalam. Hebu fikiria amecheza dhidi ya timu bora barani Afrika katika michuano ya kufuzu kombe la mataifa halafu unadai haendani na mfumo. ”

Juuko aliyesainiwa na Simba akitokea klabu ya Sports Victoria University ya nchini kwao Uganda amejikuta akisugua benchi  katika mechi za ligi na zile za kirafiki tangu mwishoni mwa msimu uliopita.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

KAMATI YA TUZO IMEFANYA MCHUJO KWENYE WACHEZAJI 30 WAMEBAKI 15, MKUDE, AJIBU WAMETOLEWA, ANGALIA ORODHA

Kamati ya Tuzo za Ligi Kuu ya Vodacom (VPL), iliyokutana wiki hii imeteua wachezaji 15 kwa ajili ya kuwania Tuzo ya Mchezaji Bora wa VPL msi...

TIBA YA KIIMANI

TIBA YA KIIMANI

a

a
Adbox