KLABU ya Aston Villa
imetangaza kuwa Roy Keane amejiuzulu wadhifa wake wa kocha wa msaidizi
wa timu hiyo. Mapema Keane alikaririwa akidai kuwa anapata tabu
kuhudumia vibarua viwili alivyokuwa navyo. Keane ambaye
pia
ni kocha msaidizi wa Ireland amesema sio haki kwa pande zote mbili,
hivyo anatakiwa kufanya uamuzi wa kuchagua kibarua kimoja. Kocha wa
Villa Paul Lambert alithibitisha asubuhi ya leo kuwa taarifa hizo na
kudai kuwa ana heshimu uamuzi uliochukuliwa.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni