Chama cha soka nchini England (FA) kimewatoza Chelsea na West Ham adhabu ya £50,000 (Chelsea) na £40,000 (West Ham) kwa kushindwa kuwadhibiti wachezaji wao kwenye ya iliyopita ya Premier League wakati vilabu hivyo vilipoumana Upton Park.
Vilabu vyote viwili vimekiri mashtaka hay ya FA ya utovu wa nidhamu na wameonywa kutorudia tena tabia hiyo.
Mechi hiyo iliisha kwa West Ham kushinda kwa 2-1 ambapo kiungo wa Chelsea, Nemanja Matic alitolewa kwa kadi nyekundu kabla ya mapumziko.
Bosi wa Chelsea Jose Mourinho na kocha wake msaidizi Silvino Louro wote walitolewa kwenye benchi la ufundi baada ya kukwaruzana na mwamuzi Jonathan Moss.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni