MSHAMBULIAJI
Zlatan Ibrahimovic ameshinda tuzo ya Mchezaji Bora wa Mwaka wa Sweden
kwa mara ya 10 katika historia yake na mara ya tisa mfululizo.
Na
baada ya ushindi wa tuzo hiyo, mchezaji huyo mwenye nguvu, amewataka
wachezaji wenzake kujitolea kila kitu katika mchezo wa mchujo wa kufuzu
wa Euro 2016 dhidi ya Denmark.
Ibrahimovic akiwa na Figo
Mpachika mabao huyo wa Paris St Germain alikuwa ana mwaka mzuri uliopita, akishinda taji la Ligi Kuu ya Ufaransa, Ligue 1 likiwa taji lake la 12 la ligi kushinda huku akifunga mabao 30 katika mechi 35.

Mshambuliaji
huyo wa zamani wa Inter Milan na Barcelona mwenye umri wa miaka 34,
wiki hii atakuwa na mtihani mgumu kwa ajili ya taifa lake,
atakapoipigania Sweden tiketi ya Fainali za Mataifa ya Ulaya mwakani
watakapomenyama na Denmark katika mchezo wa mwisho wa kufuzu.
REKODI KATIKA TUZO HIZO ;
REKODI KATIKA TUZO HIZO ;
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni