Urusi imeahidi kushirikiana na mamlaka ya kupambana na matumizi ya dawa
za kusisimua misuli na shirikisho la riadha la kimataifa baada ya ripoti
ya WADA iliyoituhumu nchi hiyo kwa ufisadi katika riadh.
Taarifa ya wizara ya michezo ya Urusi imesema tume huru iliyoundwa na
shirika la kupambana na matumizi ya dawa za kuongeza misuli nguvu
ilifanya kazi nyingi na kuwa mapendekezo yake yataisaidia Urusi kuimarisha zaidi mifumo yake ya kupambana na uovu huo.
Imesema wizara ya michezo itatathmini kwa makini matokeo ya uchunguzi huo na ushahidi uliopatikana ili kuona namna inaweza kuchukua hatua zinazostahili.
Shirikisho la Riadha Duniani limeitaka Urusi, ifikapo mwishoni mwa wiki, kujibu tuhuma za kuhusiaka na dawa za kusisimua misuli. Rais wa Shirikisho la Riadha Duniani IAAF Sebastian Coe ametoa agizo hilo baada ya ripoti ya WADA.
Coe amesema shirikisho hilo litaangalia njia mbalimbali kufuatia ripoti iliyotolewa Shirikisho la kupambana na matumizi ya dawa ya kusisimua misuli WADA kuhusiana na wanariadha wa Urusi na matumizi ya dawa hizo.
Coe, amewakata kwa haraka wajumbe wa mamlaka iliyopo kufikiria kuliwekea vikwazo shirikisho la riadha nchini Urusi ikiwemo kusitishwa uanachama wake: Rais huyo pia amesema hatasita kupambana na mapungufu yoyote yatakayojitokeza kama taasisi hiyo.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni