STAY WITH US

LightBlog

Breaking

TANGAZA NASI: +255 655 442 255

TANGAZA NASI: +255 655 442 255

CHANZI OPEN SCHOOL

CHANZI OPEN SCHOOL

Jumanne, 2 Desemba 2014

SAMATA, ULIMWENGU, NGASA, MKUDE, ABUBAKAR KUGOMBEA TUZO YA GOAL.

MTANDAO maarufu wa habari za michezo wa Goal umetangaza majina matano ya wachezaji wa Tanzania watakaogombea tuzo ya mchezaji bora wa mwaka wa Tanzania kwa mwaka huu. Majina hayo matano yaliyotangazwa ni ya wachezaji waliofanya vyema aidha katika vilabu vyao au timu ya taifa-Taifa Stars kwa mwaka huu. Miongoni mwa maji yaliyoteuliwa ni Mbwana Samata anayecheza katika klabu ya TP Mazembe ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo-DRC ambaye amekuwa na mwa mzuri kwa kuisaidia timu yake kutinga nusu fainali ya michuano ya Klabu Bingwa barani Afrika. Wengine waliopo katika orodha hiyo ni Mrisho Ngasa anayekipiga katika klabu ya Yanga ambaye alikuwa mfungaji anayeongoza kwa mabao katika michuano ya Klabu Bingwa Afrika msimu uliopita na Salum Abubakar wa klabu ya Azam na mchezaji bora wa mwezi Octoba wa Ligi Kuu Tanzania Bara. Huku Thomas Ulimwengu anayecheza pia TP Mazembe na Jonas Mkude anayecheza Simba wakiwa nyota wengine wanaokamilisha orodha hiyo. Wasomaji wa mtandao huo watapata nafasi ya kujadili ni mchezaji gani wanaeamini kuwa mshindi kupitia mitandao ya kijamii ya facebook na twitter ambapo zoezi la upigaji kura linatarajiwa kumalizika Ijumaa Desemba 5 mwaka huu.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

KAMATI YA TUZO IMEFANYA MCHUJO KWENYE WACHEZAJI 30 WAMEBAKI 15, MKUDE, AJIBU WAMETOLEWA, ANGALIA ORODHA

Kamati ya Tuzo za Ligi Kuu ya Vodacom (VPL), iliyokutana wiki hii imeteua wachezaji 15 kwa ajili ya kuwania Tuzo ya Mchezaji Bora wa VPL msi...

TIBA YA KIIMANI

TIBA YA KIIMANI

a

a
Adbox