MSHAMBULIAJI nyota wa
Real Madrid, Cristiano Ronaldo amesema kikosi cha sasa ni kama familia
yake ya pili na anadhani hali katika vyumba vya kubadilishia nguo ni
nzuri ambayo hajawahi kuiona kwa miaka kadhaa. Nyota huyo ambaye
ameteuliwa miongoni mwa wachezaji watatu watakaogombea tuzo ya Ballon
d’Or sambamba na Lionel Messi na Manuel Neuer amekuwa katika kiwango
bora msimu huu. Ronaldo amefunga mabao 26 katika mechi 20 za mashindano
yote alizocheza huku akishuhudia klabu yake ikivunja rekodi ya kucheza
mechi 16 bila kufungwa. Akihojiwa Ronaldo amesema Madrid imekuwa kama
familia yake ya pili kwani amekuwa akifanya nao kazi kila siku na
anafurahia kuwa pamoja na wachezaji wenzake.
TANGAZA NASI: +255 655 442 255
CHANZI OPEN SCHOOL
Jumanne, 2 Desemba 2014
MADRID NI KAMA FAMILIA YANGU YA PILI - RONALDO.
About asantemuya
Soratemplates is a blogger resources site is a provider of high quality blogger template with premium looking layout and robust design. The main mission of templatesyard is to provide the best quality blogger templates.
Jisajili kwenye:
Chapisha Maoni (Atom)
KAMATI YA TUZO IMEFANYA MCHUJO KWENYE WACHEZAJI 30 WAMEBAKI 15, MKUDE, AJIBU WAMETOLEWA, ANGALIA ORODHA
Kamati ya Tuzo za Ligi Kuu ya Vodacom (VPL), iliyokutana wiki hii imeteua wachezaji 15 kwa ajili ya kuwania Tuzo ya Mchezaji Bora wa VPL msi...
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni