STAY WITH US

LightBlog

Breaking

TANGAZA NASI: +255 655 442 255

TANGAZA NASI: +255 655 442 255

CHANZI OPEN SCHOOL

CHANZI OPEN SCHOOL

Ijumaa, 30 Januari 2015

AFCON 2015: CAF KUANGALIA UPYA UTARATIBU WA KUPATA MSHINDI KWA BAHATI NASIBU ULIOWATOA MALI JANA.


SHIRIKISHO la Soka la Afrika-CAF limesema litaupitia upya utaratibu wa kumpata mshindi kwa njia ya bahati nasibu baada ya timu kuwa sawa katika hatua ya makundi. Hatua hiyo inakuja kufuatia jana Guinea kutinga robo fainali kwa ushindi wa mezani baada ya kubahatika kwenye bahati nasibu hiyo huku Mali ikifungasha virago baada ya timu zote mbili kumaliza mechi za makundi zikiwa zote zina alama tatu sawa na mabao matatu ya kufunga. Katika mechi za kundi D zilizomalizika juzi ni Ivory Coast pekee ndio waliokuwa wamesonga mbele baada ya kuifunga Cameroon kwa bao 1-0. Wadau wengi na mashabiki wa soka wameukosoa utaratibu huo wa bahati nasibu wakidai kuwa hautendi haki. Mkurugenzi wa habari wa CAF Junior Binyam amesema pamoja na kwamba walipaswa kusimamia kanuni za mashindano hayo lakini anadhani ipo haja ya kuboresha utaratibu wa kumpata mshindi pindi tukio kama hilo linapotokea. Binyam aliendelea kudai kuwa sio haki kwa timu kurudi nyumbani kama ilivyofanyika kwa Mali

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

KAMATI YA TUZO IMEFANYA MCHUJO KWENYE WACHEZAJI 30 WAMEBAKI 15, MKUDE, AJIBU WAMETOLEWA, ANGALIA ORODHA

Kamati ya Tuzo za Ligi Kuu ya Vodacom (VPL), iliyokutana wiki hii imeteua wachezaji 15 kwa ajili ya kuwania Tuzo ya Mchezaji Bora wa VPL msi...

TIBA YA KIIMANI

TIBA YA KIIMANI

a

a
Adbox