Mama mzazi wa mtoto wa Cristiano Ronaldo amefahamika kuwa ni mwanafunzi wa Uingereza....ambaye sasa anamtaka mtoto wake.
Mpaka
sasa Ronaldo ameficha siri ya jina, umri na hata Utaifa wa mzazi
mwenzake kufuatia kupata haki ya kumiliki mtoto kwa malipo ya paundi
milioni 10.
Hata
hivyo, Gazeti la Sunday Mirror limeweka wazi kuwa mwanamke huyo ana
umri wa miaka 20 ambaye anajutia maamuzi yake na amekuwa akimpigia simu
mara nyingi nyota huyo wa zamani wa Manchester United akiomba nafasi ya
kuonana na mtoto wake.
Mwanamke
huyo aliyepata ujauzito kwa kulala na Ronaldo usiku mmoja anadai yuko
tayari hata kulipa mamilioni aliyopewa, akisisitiza amebadili akili
yake.
Maamuzi
yake ya kumpa mtoto Ronaldo, mchezaji ghali katika historia ya mpira
yamemuacha awe na msongo wa mawazo, marafiki zake wanasema, hali hiyo
imesababisha ashuke kiwango kitaaluma.
Kipengele
cha mkataba alichosaini na mwanasheria wa Ronaldo kinamaanisha
haruhusiwi kumuambia mtu yeyote kuwa yeye ndiye mama mzazi wa mtoto wake
ikiwemo na familia yake.
Alipotea baada ya kupata mimba na baada ya kuzaa aliwaambia watu alipata matatizo kidogo ya kuvimba tumbo.
Alipoomba kumona mwanaye, Ronaldo alisema anafirikiria ombi lake kama atarudisha baadhi ya pesa alizopewa.
Chanzo
cha karibu cha mwanamke huyo kilisema: "Mara nyingi usiku anampigia
Ronaldo. Anamlilia sana na kumbembeleza. Ronaldo hakuwa hata na
mawasiliano naye, lakini kwasasa wanaongea kwenye twita"
"Anampigia
hata baada ya mechi akimpongeza kwa jinsi alivyocheza, akiamini kwamba
siku moja atakata rufaa, lakini Ronaldo anamtia moyo kuhusu kumuona
Cristiano Jr.
"Mwanamke
huyu anahisi kama ameuza roho yake. Ana maisha ya kimilionea, lakini
kamwe hawezi hata kumwabia rafiki yake na familia ukweli kuhusu
kilichotokea---hakika kitendo hiki kinamfanya awe mpweke".
Rafiki
wa Ronaldo ambaye ana miaka 29 sasa alisema "Kwa vile hilo lilikuwa juu
yake, lilikuwa chaguo lake, maamuzi yake. Alisema, "Hana haki yoyote
juu ya mtoto wangu. Hatamwona tena mwanangu"
"Lakini
Ronaldo anapokea simu zake, ana wasiwasi kuwa anaweza kupambana kupata
haki ya kumuona mwanaye na anataka kusikia anawaza nini"
"Kwa
mkataba uliosainiwa unamkaba kabisa. Lakini ana nguvu kama mama ya
kupata haki ya kumuona mwanaye--kwahiyo kitu chochote kinaweza kutokea".
Marafiki
wa Ronaldo wanasema, nyota huyo wa Real Madrid alikutana na mwanamke
huyo katika klabu ya usiku mjini London na walifanya mapenzi katika
hoteli.
Alipokuwa na mimba aliwasiliana na Ronaldo kupitia wakala wake Jorge Mendes na mambo mengine yalipigwa chini.
Mama yake Ronaldo mwenye miaka 58 Doleres na dada zake Elma na Liliana Catia walikubali kumlea mtoto huyo.
Baada
ya mtoto kuzaliwa, mwanasheria wa Ronaldo alifanya mpango wa vipimo vya
DNA kuthibitisha kama kweli mtoto ni wa nyota huyo raia wa Ureno.
Jambo hili lilifanyika majira ya kiangazi mwaka 2010 wakati nyota huyo aliyerithi jezi namba saba ya George Best, Eric Cantona na David Beckham akiwa Man Utd, anacheza fainali za kombe la dunia nchini Afrika kusini.
Julai
3 mwaka huo,Ronaldo aliitangazia dunia kuwa ana mtoto wa kiume,
aliandika kwenye ukurasa wa facebook kuwa mama yake hataki
kutambulishwa. Aliongeza: "Mwanangu atakiwa chini ya uangalizi wangu"
Vyombo
vya habari vilimsakama Ronaldo vikitaka kujua jina la mama mzazi wa
mtoto ikiwemo Paris Hilton na Realiy TV Star Imogen Thomas, lakini kamwe
jina lake halikuwekwa wazi.
Kwa
mara ya kwanza mtoto alioneshwa hadharani desemba 8, 2011 nchini
Hispania katika mechi ya Real Madrid ambapo mama yake Ronaldo na ndugu
zake walipiga picha wakiwa wamembeba.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni