MENEJA wa klabu ya
Chelsea, Jose Mourinho anaamini kikosi chake kingeweza kuichapa
Tottenham Hotspurs kama wangezawadiwa penati ambayo ingewafanya kuongoza
katika mchezo huo. Baada ya Diego Costa kuifungiwa Chelsea bao la
kuongoza, timu hiyo ilinyimwa penati na mwamuzi Phil Dowd wakati Jan
Vertonghen aliposhika mpira katika eneo la hatari, na baadae kuja
kupoteza mchezo huo kwa kufungwa mabao 5-3. Mourinho alimlaumu mwamuzi
wa mchezo huo kwa kushindwa kutoa penati hiyo kwani ingewapa nafasi
nzuri ya kushinda mchezo huo. Hata hivyo baadhi wachambuzi wa soka
wameshindwa kukubaliana na Mourinho wakidai kuwa haikustahili kuwa
penati hivyo mwamuzi alikuwa sahihi. Chelsea ambao walikuwa wakiongoza
kwa tofauti ya alama nane katika msimamo wa Ligi Kuu Novemba mwaka jana
sasa wako juu ya Manchester City kutokana na mpangilio wa herufi
kufuatia kipigo hicho cha jana.
TANGAZA NASI: +255 655 442 255
CHANZI OPEN SCHOOL
Ijumaa, 2 Januari 2015
Home
/
Unlabelled
/
KAMA KAWAIDA YAKE MOURINHO ALIA NA WAAMUZI BAADA YA KICHAPO CHA 5-3 KUTOKA KWA SPURS.
KAMA KAWAIDA YAKE MOURINHO ALIA NA WAAMUZI BAADA YA KICHAPO CHA 5-3 KUTOKA KWA SPURS.
About asantemuya
Soratemplates is a blogger resources site is a provider of high quality blogger template with premium looking layout and robust design. The main mission of templatesyard is to provide the best quality blogger templates.
Jisajili kwenye:
Chapisha Maoni (Atom)
KAMATI YA TUZO IMEFANYA MCHUJO KWENYE WACHEZAJI 30 WAMEBAKI 15, MKUDE, AJIBU WAMETOLEWA, ANGALIA ORODHA
Kamati ya Tuzo za Ligi Kuu ya Vodacom (VPL), iliyokutana wiki hii imeteua wachezaji 15 kwa ajili ya kuwania Tuzo ya Mchezaji Bora wa VPL msi...
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni