KATIKA habari za tetesi
za usajili zilizopamba vichwa vya habari katika mitandao na magazeti
barani Ulaya, mojawapo ni klabu za Chelsea na Manchester United
zimepashwa kuwa zitalazimika kulipa kitita cha paundi milioni 20 kama
watahitaji sahihi ya beki wa Real Madrid Raphael Varane. Kwingineko
klabu ya Liverpool inajipanga kuilipa kitita cha paundi milioni tatu
klabu ya Lille kwa ajili ya kumrejesha mshambuliaji Divock Origi mwezi
huu. Chipukizi huyo mwenye umri wa miaka 19 sasa yuko katika mkataba wa
msimu mzima na klabu hiyo ya Ufaransa. Meneja wa Manchester City Manuel
Pellegrini anataka kumsajili kiungo wa klabu ya Schalke Julian Draxler
ingawa klabu hiyo ya ujerumani inataka kitita cha paundi milioni 25 kwa
ajili ya mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 21. Kiungo mkongwe wa klabu
ya Liverpool, Steven Gerrard mwenye umri wa miaka 34 amepiga chini ofa
yenye thamani ya paundi milioni 18 kwa ajili ya kwenda kucheza soka
nchini Qatar wakati atakapoondoka Anfield mwishoni mwa msimu
huu. Tukibakia hapohapo Anfield, Liverpool inatarajia kutenga kitita cha
paundi milioni 23 kwa ajili ya mshambuliaji wa klabu ya West Bromwich
Albion Saido Berahino mara watakapomuuza Fabio Borin. Kwa upande wa
Tottenham Hostpurs wao wanaripotiwa kujiandaa kumuuza golikipa wao Hugo
Lloris mwenye umri wa miaka 28 kwa kitita cha paundi milioni 25. Nchini
Hispania kiungo mahiri wa Barcelona Sergio Busquets mwenye umri wa miaka
26 anajipanga kuzinyong’onyesha klabu za Arsenal, Chelsea na Manchester
United zinzomuwinda, kwa kusaini mkataba mpya na kllabu hiyo.
TANGAZA NASI: +255 655 442 255

CHANZI OPEN SCHOOL

Jumatatu, 5 Januari 2015
Home
/
Unlabelled
/
TETESI ZA USAJILI ULAYA: MADRID KUMUACHIA VARANE KWA PAUNDI MILIONI 20, LIVERPOOL KUMREJESHA ORIGI, CITY YAMPIGIA HESABU DRAXLER.
TETESI ZA USAJILI ULAYA: MADRID KUMUACHIA VARANE KWA PAUNDI MILIONI 20, LIVERPOOL KUMREJESHA ORIGI, CITY YAMPIGIA HESABU DRAXLER.
About asantemuya
Soratemplates is a blogger resources site is a provider of high quality blogger template with premium looking layout and robust design. The main mission of templatesyard is to provide the best quality blogger templates.
Jisajili kwenye:
Chapisha Maoni (Atom)
KAMATI YA TUZO IMEFANYA MCHUJO KWENYE WACHEZAJI 30 WAMEBAKI 15, MKUDE, AJIBU WAMETOLEWA, ANGALIA ORODHA
Kamati ya Tuzo za Ligi Kuu ya Vodacom (VPL), iliyokutana wiki hii imeteua wachezaji 15 kwa ajili ya kuwania Tuzo ya Mchezaji Bora wa VPL msi...

TIBA YA KIIMANI

a

Hakuna maoni:
Chapisha Maoni