Wachezaji wa Simba ambao walishiriki katika
kikosi kilichoing’oa Zamalek mwaka 2003 wameamua kumchangia mwenzao Christoper
Alex Massawe.
Massawe yu mgonjwa taabani kwao Dodoma. Hali
ambayo imewafanya Simba walioifunga Zamalek, Massawe akifunga penalti ya mwisho
iliyoihakikishia Simba ushindi.
Kiungo huyo anaumwa na imeelezwa
anasumbuliwa na kifua kikuu ingawa bado jambo hilo halijatolewa ufafanuzi na
familia yake.
Boniface Pawasa
ambaye alicheza namba tano katika mechi hiyo amesema wanaandaa mechi ya
kirafiki.
“Lengo ni kupata mechi ambayo itamsaidia
ndugu yetu kupata matibabu.
“Wikiendi hii tunaweza kucheza pale Karume
kama hakutakuwa na mechi ya daraja la kwanza. Hili ni jukumu letu, wadau
wajitokeze.
“Tayari baadhi ya waliocheza siku hiyo wamejitokeza, Emmanuel Gabriel na Victor Costa tumeishakubaliana," alisema.
Credit: Saleh Jembe
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni