STAY WITH US

LightBlog

Breaking

TANGAZA NASI: +255 655 442 255

TANGAZA NASI: +255 655 442 255

CHANZI OPEN SCHOOL

CHANZI OPEN SCHOOL

Jumanne, 19 Aprili 2016

PSG KUIFANYIA UMAFIA MAN UNITED KWA MOURINHO.

KLABU ya Paris Saint-Germain-PSG inadaiwa kuwa katika mazungumzo na meneja wa zamani wa Chelsea, Jose Mourinho. 
 
PSG tayari wameshanyakuwa taji la La Liga msimu huu na wako katika nafasi nzuri ya kutwaa taji la Kombe la Ligi na Kombe la Ufaransa, hata hivyo lengo lao kubwa lilikuwa ni kuvuka hatua ya robo fainali ya michuano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya. 
 
Kufuatia kuenguliwa katika michuano hiyo ya Ulaya na Manchester City, meneja wa klabu hiyo Laurent Blanc amekuwa katika hatari ya kutimuliwa kufuatia taarifa hizo. 
 
Mourinho amekuwa akihusishwa na tetesi za kwenda Manchester United kwa kipindi kirefu lakini uwezekano wa timu hiyo kufuzu michuano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya msimu ujao unaweza kumfanya Louis van Gaal kuendelea na kibarua chake. 
 
PSG walipotafutwa kutoa kauli yao kuhusiana na taarifa hizo walikataa kusema chochote.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

KAMATI YA TUZO IMEFANYA MCHUJO KWENYE WACHEZAJI 30 WAMEBAKI 15, MKUDE, AJIBU WAMETOLEWA, ANGALIA ORODHA

Kamati ya Tuzo za Ligi Kuu ya Vodacom (VPL), iliyokutana wiki hii imeteua wachezaji 15 kwa ajili ya kuwania Tuzo ya Mchezaji Bora wa VPL msi...

TIBA YA KIIMANI

TIBA YA KIIMANI

a

a
Adbox