AZAM
FC imeshinda mechi ya tatu mfululizo ya kirafiki, baada ya kuilaza
mabao 2-1 JKT Ruvu Stars Uwanja wa Azam Complex, Chamazi, Dar es Salaam,
wachezaji wa kigeni wakiendelea kuibeba timu.
Mabingwa hao wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara, walikwenda kupumzika wakiwa tayari wanaongoza tayari kwa mabao 2-0, yaliyotiwa kimiani na Mrundi Didier Kavumbangu na Kipre Tchetche kutoka Ivory Coast.
Kipindi
cha pili, kocha Mcameroon, Joseph Marius Omog alibadilisha karibu
wachezaji wote walioanza na JKT Ruvu ya Freddy Felix Minziro ilitumia
mwanya huo kujipatia bao la kusawazisha lililofungwa na Hassan Bilal,
aliyemalizia kazi nzuri ya Betram Mombeki.
Mshambuliaji mpya wa Azam FC kutoka Haiti, Leonel Saint- Preux alicheza vizuri na ndiye aliyetoa pasi ya bao la pili, wakati Ismaila Diara kutoka Mali alikuwa jukwaani kabisa kutokana na mejeruhi.
Chipukizi
waliopandishwa kutoka akademi, Abdul Mgaya, Bryson Raphael, Malik
Farid, Dizana Issa na Mudathir Yahya ambao walianza kipindi cha kwanza,
wote walicheza vizuri.
Awali, Azam FC ilizifunga kombaini ya Jeshi 3-2, mabao yake yakifungwa Ismaila Diara mawili na Mudathir Yahya moja, kabla ya kuilaza Polisi Morogoro 1-0, bao pekee la Leonel Saint- Preux.
Mabingwa hao wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara, walikwenda kupumzika wakiwa tayari wanaongoza tayari kwa mabao 2-0, yaliyotiwa kimiani na Mrundi Didier Kavumbangu na Kipre Tchetche kutoka Ivory Coast.
Mshambuliaji wa Azam FC, Didier Kavumbangu akimiliki mpira mbele ya beki wa JKT Ruvu, Mohammed Fakhi leo Chamazi |
Mshambuliaji wa Azam Lionel Saint- Preux akipasua katikati ya mabeki wa JKT Ruvu, Fakhi kulia na Nafo Sasane kushoto |
Mshambuliaji wa Azam FC, Kipre Tchetche akimtoka beki wa JKT Ruvu, Haruna Shamte |
Kiungo wa Azam FC, Bryson Raphael akifumua shuti pembeni ya Hassan Bilal wa JKT Ruvu |
Beki chipukizi wa Azam FC, Abdul Mgaya akiondosha mpira mbele ya mshambuliaji wa JKT Ruvu, Betram Mombeki |
Mshambuliaji mpya wa Azam FC kutoka Haiti, Leonel Saint- Preux alicheza vizuri na ndiye aliyetoa pasi ya bao la pili, wakati Ismaila Diara kutoka Mali alikuwa jukwaani kabisa kutokana na mejeruhi.
Didier Kavumbangu akipiga mpira mbele ya beki wa JKT Ruvu, Mohammed Fakhi |
Katibu wa Azam FC, Nassor Iddirsa kulia akiangalia muda wakati mchezo huo ukielekea ukingoni |
Awali, Azam FC ilizifunga kombaini ya Jeshi 3-2, mabao yake yakifungwa Ismaila Diara mawili na Mudathir Yahya moja, kabla ya kuilaza Polisi Morogoro 1-0, bao pekee la Leonel Saint- Preux.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni