STAY WITH US

LightBlog

Breaking

TANGAZA NASI: +255 655 442 255

TANGAZA NASI: +255 655 442 255

CHANZI OPEN SCHOOL

CHANZI OPEN SCHOOL

Alhamisi, 17 Julai 2014

WACHEZAJI YANGA KUAGA ULOFA, WOTE KUNUNULIWA NYUMBA


10520854_764099123654035_8662161622159735181_n 
KLABU ya Yanga imeingia makubaliano ya kununua nyumba za Shirika la Hifadhi ya Jamii (NSSF), kwa ajili ya wachezaji wake kupitia program maalumu.
Akizungumza katika hafla ya utiaji saini makubalinao hayo iliyofanyika jana katika Hoteli ya Serena, Mkurugenzi wa Huduma na Uendeshaji wa NSSF, Crecentius Magori alisema wachezaji wanapaswa kuona fahari kumiliki nyuma au ardhi mjini, si magari.
Magori alitumia fursa hiyo kuwahamasisha wachezaji wa Yanga ambao walikuwepo katika utiaji wa saini makubaliano hayo, kuchangamkia mradi huo uliopo makao mapya katika Kijiji cha Dege, Kigamboni, jijini Dar es Salaam.
“Sisi tuko tayari kuwapa fomu na kwenda kuwaonyesha nyumba hizo za kisasa zaidi, hivyo ningependa kuwashauri mpatapo fedha za mikataba, mkitoa kiasi nanyi muwe wamiliki wa nyumba hizo. “Kama utamudu na kutoa kiasi cha sh. mil.8 na kulipa kwa miezi mitatu mfululizo, NSSF watawapa ufunguo na kuendelea kulipa kila mwisho wa mwezi kwa miaka 15, kisha unakuwa mmiliki halali wa nyumba hiyo,” alisema Magori. Aliongeza kuwa hata ikitokea mchezaji akafariki dunia, nyumba hiyo itaendelea kuwa mali ya familia ya mhusika kwani itakuwa imerithiwa huku akisihi wachezaji ambao si wanachama wa NSSF, kujiunga ili kupata manufaa ya shirika hilo. Akizungumza katika hafla hiyo, Katibu Mkuu wa Yanga, Beno Njovu, alisema makubaliano hayo ni matokeo ya mazungumzo kati ya Mwenyekiti wa klabu hiyo, Yusuf Manji na Mkurugenzi Mkuu wa NSSF, Dk. Ramadhan Dau. 
Alisema lengo ni kuhakikisha kila mchezaji wa timu hiyo anawezeshwa kumiliki nyumba ikiwa ni moja ya mali ya kudumu ambayo itakuwa na manufaa yake wakati anacheza, hata baada ya kustaafu soka
KATIBU MKUU WA YANGA, BENO NJOVU, ALIKUWEPO.
MAXIMO, MSAIDIZI WAKE LEIVA, SALVATORY EDWARD WAKISIKILIZA KWA UMAKINI MKUBWA.
MPOGOLO NA JACOB, WALIKUWEPO.
BAADHI YA MIJENGO.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

KAMATI YA TUZO IMEFANYA MCHUJO KWENYE WACHEZAJI 30 WAMEBAKI 15, MKUDE, AJIBU WAMETOLEWA, ANGALIA ORODHA

Kamati ya Tuzo za Ligi Kuu ya Vodacom (VPL), iliyokutana wiki hii imeteua wachezaji 15 kwa ajili ya kuwania Tuzo ya Mchezaji Bora wa VPL msi...

TIBA YA KIIMANI

TIBA YA KIIMANI

a

a
Adbox