Mchezaji
wa zamani wa Liverpool Raheem Sterling amejiunga na kikosi cha
Manchester City baada ya kupambana kwa muda mrefu kuihama klabu hiyo kwa
madai kwamba anahitaji kucheza kwenye timu ambayo anaweza kutwaa
mataji. Liverpool imekuwa na ukame wa mataji kwa miaka ya hivi karibuni,
msimu uliomalizika ‘majogoo wa jiji’ walimaliza wakiwa nafasi ya sita
wakiwa na pointi 64 na hiyo inamaanisha hawana nafasi ya kushiriki
michuano ya vilabu bingwa barani Ulaya ambayo kila mchezaji anatamani
kucheza.
Sababu
kubwa ya Sterling kuikacha Liverpool ni ukame wa mataji unaoiandama
klabu hiyo, nyota huyo wa kimataifa wa England anaamini kuwa kwa sasa
yupo kwenye kiwango bora hivyo anahitaji kuwa kwenye klabu
itakayomuwezesha kutwaa vikombe.
Kuna
wachezaji wengi ambao waliondoka Liverpool miaka ya hivi karibuni na
wakafanikiwa kutwaa makombe ikiwemo la UEFA Champions League ambalo ndio
kombe kubwa (lenye hadhi ya juu) kwa ngazi ya vilabu barani Ulaya.
Hii
ni orodha ya wachezaji watano ambao waliondoka Liverpool kwa nyakati
tofauti na kufanikiwa kutwaa vikombe wakiwa na vilabu vingine.
Fernando Torres-Chelsea
Alvaro Arbeloa-Real Madrid
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni