MABINGWA wa zamani wa Tanzania na Afrika Mashariki na Kati, Simba SC wanatarajiwa kurejea leo Dar es Salaam kutoka Lushoto, Tanga walipokuwa wameweka kambi kwa wiki mbili zilizopita.
Simba SC wamemua kuvunja kambi yao ya Lushoto, kufuatia taarifa za kusogezwa mbele kwa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara kutoka Agosti hadi Septemba.
Kikosi cha Simba SC kinachotarajiwa kurejea Dar es Salaam ni makipa; Peter Manyika
David
Robert Kisu, Denis Deonis Richard na Ivo Mapunda, mabeki, Mohammed
Hussein ‘Tshabalala’, Hassan Ramadhani ‘Kessy’, Samih Hajji Nuhu, Hassan
Isihaka, Murushid Juuko na Mohamed Fakih Khatib.
Viungo ni Jonas Mkude, Said Ndemla,
Abdi Banda, Awadh Juma, Simon Sserenkuma, Peter Mwalyanzi na washambuliaji Mussa Hassan Mgosi, Ibrahim Hajib, Hamisi Kiiza, Elias Maguli, Issa Abdallah Ngoa, Emmanuel Alex Massawe, Michael Mgimwa, Mbaruku Yusuph na Saidi Issa.
Benchi la ufundi limeongozwa na kocha Mkuu, Dylan Kerr, Kocha Msaidizi, Suleiman Matola, Kocha wa makipa Iddi Salim Abdul, Kocha wa viungo, Dusan Momcilovic na Daktari Yassin Gembe.
Simba SC watatua Dar es Salaam wakati michuano ya Klabu Bingwa Afrika Mashariki na Kati, Kombe la Kagame inaanza kesho, wenyeji Tanzania Bara wakiwakilishwa na Yanga SC na Azam FC.
Kufanya vibaya kwa Simba SC kwa miaka mitatu iliyopita katika Ligi Kuu, kumewafanya siyo tu wakose nafasi ya kucheza Kombe la Kagame, bali hata michano ya Afrika, yaani Kombe la Washindi na Ligi ya Mabingwa.
Lakini msimu huu, chini ya Rais wake, Evans Elieza Aveva- Simba SC imepania kurejesha heshima.
Lakini inawezekana kikosi hicho cha Kocha Muingereza, Dylan Kerr kikaendelea na mazoezi hapa hapa Dar es Salaam.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni