STAY WITH US

LightBlog

Breaking

TANGAZA NASI: +255 655 442 255

TANGAZA NASI: +255 655 442 255

CHANZI OPEN SCHOOL

CHANZI OPEN SCHOOL

Jumanne, 19 Aprili 2016

AZAM YACHEZEA KICHAPO MBELE YA ESPERANCE....................

Wachezaji wa kikosi cha Azam wakihamasishana kabla ya kuanza kwa mechi yao dhidi ya Esperance  

AZAM FC imeaga michuano ya Kombe la Shirikisho la Soka Afrika baada ya kufungwa mabao 3-0 na wenyeji Esperance katika mchezo wa marudiano hatua ya 16 Bora usiku wa leo Uwanja wa Olimpiki Novemba 7 mjini Rades, Tunis, Tunisia.

Himid Mao (kulia) lakini aliingia badaye dakika ya 79, Mao pia hakucheza kabisa kwenye mchezo wa awali uliozikutanisha klabu hizo jijini Dar es Salaam Himid Mao (kulia) lakini aliingia badaye dakika ya 79, Mao pia hakucheza kabisa kwenye mchezo wa awali uliozikutanisha klabu hizo jijini Dar es Salaam
  Matokeo hayo yanafanya Azam FC inayomilikiwa na bilionea Alhaj Sheikh Said Salim Awadh Bakhresa na familia yake itolewe kwa jumla ya mabao 4-2, baada ya awali kushinda 2-1 Dar es Salaam.
  Ikicheza mchezo wa kujihami kwa kutumia viungo watano na mshambuliaji mmoja tu, Nahodha John Rapahel Bocco, Azam ilifanikiwa kuwabana vizuri wenyeji dakika 45 za kwanza na kumaliza bila kuruhusu bao.


Allan Wanga (wa kwanza kushoto) na wachezaji wengine wa Azam wakiwa benchi, mchezaji huyo wa Kenya amekuwa na wakati mgumu kwenye kikosi cha Azam kutokana na kukosa kabisa nafasi ya kuanza kwenye kikosi cha kwanza cha Azam  

Timu hiyo ya kocha Muingereza, Stewart John Hall ilikuwa ikifanya mashambulizi ya kushitukiza kwa kumpelekea mipira mirefu Bocco, ambaye hata hivyo alidhibitiwa.
 
Ukuta wa Azam FC ulifanya kazi ya ziada ya kuzuia mashambulizi ya Esperance muda mwingi wa kipindi hicho, huku kipa Aishi Manula akiokoa michomo zaidi ya minne ya hatari langoni mwake.

 
Hata hivyo, bao la mapema kipindi cha pili walilopata Esperance lilitibua mipango yote ya timu ya Chamazi, nje kidogo ya Jiji la Dar esb Salaam.

 
Bao hilo lilifungwa na Saad Bguir dakika ya 47 kwa shuti la mpira wa adhabu umbali wa mita 19, baada ya Fakhreddine Ben Youssef kuangushwa na David Mwantika nje kidogo ya boksi.

 
Baada ya bao hilo, Azam FC walibadilisha mfumo na wao kuanza kushambulia moja kwa moja na hapo ndipo mchezo ukaanza kuwa pande zote.



 Azam-Tunis 2
 


Hata hivyo, kufunguka kwa Azam FC kuliipa nafasi Esperance ya kufanikisha mipango yake na kufanikiwa kuongeza mabao mawili.
 
Dakika ya 63 Haithem Jouini alifunga kwa kichwa akimalizia mpira uliotemwa na kipa Aishi Manula kufuatia krosi ya Hoiucine Regued na dakika ya 80 Fakhreddine Ben Youssef akafunga la tatu akimalizia pasi ya kiungo Driss Mhirsi.

 
Azam haikuweza kabisa kulitia misukosuko lango la Esperance ambao walikuwa wanafurahia uchezeshaji wa marefa wa nchi jirani yao, Morocco.



 Juma lililopita kuna taarifa zilitoka zikisema Farid Musa amesafiri kuelekea Hispania kufanya majaribio kwenye klabu moja ya kuko, lakini alionekana kwenye kikosi cha Azam kilichocheza dhidi ya Esperance na kuzua maswali mengi kwa watu
 
Kwa ujumla katika mchezo wa leo, Azam ilionekana kabisa kuathiriwa na kuwakosa wachezaji wanne tegemeo, mabeki Shomary Kapombe ambaye ni mgonjwa, Serge Wawa majeruhi, kiungo Jean Baptiste Mugiraneza aliyekuwa anatumikia adhabu ya kadi na mshambuliaji Kipre Tchetche aliyekuwa majeruhi pia. 



 Ramadhani Singano (Messi) amekuwa ni msaada mkubwa kwenye kikosi cha Azam siku za usoni tangu aliojihakikishia nafasi kwenye kikosi hicho. Messi ndiye aliyefunga goli la pili dhidi ya Esperance kwenye mchezo wa kwanza uliochezwa Dar
 


Kwa matokeo hayo, Esperance itamenyana na moja ya timu nane zitakazotolewa katika 16 Bora ya Ligi ya Mabingwa Afrika kuwania kucheza hatua ya makundi ya Kombe la Shirikisho.
 
Kikosi cha Esperance kilikuwa: Moez Ben Cherifia, Iheb Mbaarki, Yacine Rabii, Mohamed Ali Yaakoubi, Chamseddine Dhaouadi, Hoiucine Regued/Chaker Rergui dk87, Fousseny Coulibaly, Driss Mhirsi, Saad Bguir/Ilyes Jelassi dk77, Fakhreddine Ben Youssef na Haithem Jouini/Bernard Bulbwa dk83.

 
Azam FC kipo; Aishi Manula, Erasto Nyoni, Waziri Salum/Himid Mao dk79, David Mwantika, Aggrey Morris, Kipre Balou, Ramadhani Singano ‘Messi’, Frank Domayo, John Bocco, Salum Abubakar ‘Sure Boy/Didier Kavumbangu dk79, Farid Mussa/Khamis Mcha dk65.  







Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

KAMATI YA TUZO IMEFANYA MCHUJO KWENYE WACHEZAJI 30 WAMEBAKI 15, MKUDE, AJIBU WAMETOLEWA, ANGALIA ORODHA

Kamati ya Tuzo za Ligi Kuu ya Vodacom (VPL), iliyokutana wiki hii imeteua wachezaji 15 kwa ajili ya kuwania Tuzo ya Mchezaji Bora wa VPL msi...

TIBA YA KIIMANI

TIBA YA KIIMANI

a

a
Adbox