Rais wa TFF, Jamal Malinzi
KAMATI
ya Utendaji ya Shrikisho la Mpira wa Miguu nchini -TFF iliyokutana
jumapili Februari 22 mwaka huu, imefanya mabadiliko ya mahali
utakaofanyika Mkutano Mkuu wa mwaka kutoka Mkoa wa Sinigida na
kuhamishia mkoa wa Morogoro.
Hatua
hiyo imefikiwa na Kamati ya Utendaji kutokana na sababu za
kutokukamilika kwa miundombinu ya mkutano mkuu na kuwepo ka shughuli
nyingine za kijamii mkoani humo.
Kamati
ya Utendaji inamshukuru Mwenyekiti wa Chama cha Mpira wa Miguu mkoa wa
Singida (SIREFA), na uongozi mzima kwa kujitolea kuandaa mkutano huo na
huko nyuma waliweza kuandaa mkutano wa makatibu wa vyama vya soka vya
mikoa.
TFF
itaandaa vikao na matukio mengine mkoani Singida itakapotokea hapo
baadae, tarehe ya mkutano mkuu itaendelea kubakia ile ile ya Machi 14,
15 mwaka huu.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni