STAY WITH US

LightBlog

Breaking

TANGAZA NASI: +255 655 442 255

TANGAZA NASI: +255 655 442 255

CHANZI OPEN SCHOOL

CHANZI OPEN SCHOOL

Jumatatu, 2 Februari 2015

YANGA SASA YAAMUA KUPAMBANA NA EBOLA, MANJI AMWAGA DOLA LAKI 5 AKITAKA MASHINDANO

KLABU ya Yanga kupitia Mwenyekiti wake Yusuf Manji imewasilisha pendekezo mbele ya Marais wanaounda Umoja wa Afrika (AU) kuanzisha mashindano maalum ya kupambana na ugonjwa wa Ebola lakini kwa kuanzia akatoa kiasi cha Dola 500,000 kwa kuanzia.
Pendekezo hilo la Manji amelitoa Alhamisi ya Januari 29 wiki iliyopita jijini Adis Ababa nchini Ethiopia kulikofanyika mkutano huo ambao kwa nchi uliwakilishwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk Jakaya Kikwete huku Manji akiwa mmoja wa wageni.
Akizungumza na waandishi wa habari leo mchana Katibu wa Yanga Jonas Dk Tibohora ambaye naye aliongozana na Manji alisema katika kikao hicho cha 24 cha AU Manji amewasilisha pendekezo hilo akitaka nchi 54 za Afrika kushiriki katika mashindano hayo mafupi kusaka fedha za kupambana na ugonjwa huo hatari unaiosumbua Afrika Magharibi kwa kuchukua washindi wawili wa juu katika kila ligi.
Tibohora amesema katika pendekezo hilo la Manji ambalo nchi zote zililiafiki Manji ametaka mashindano hayo kuchezwa kwa kanda za nchi huzika ambapo mechi hizo zitachezwa kwa mfumo wa nyumbani na ugenini huku kila klabu ikitakiwa kuchangia kiasi cha dola 100000 (shilingi mil 170) kama kiingilio.
Amesema lengo la Manji ni kutaka kuona soka linachangia katika mapambano ya ugonjwa huo ambapo jumla ya kiasi cha dola 10.8 ml zitaweza kupatikana huku mwenyekiti huyo akitangulia kutoa dola 500000 kama kianzio.
"Mwenyekiti amependekeza kwamba kwa kuwa Yanga tunaitwa Young African Football Club jina letu lifanye kitu kuhusu Afrika na kwa kuwa kila kanda za afrika mfano hii ya kwetu ya Afrika Mashariki tuna utaratibu wetu wa kumaliza msimu mashindano hayo sasa yafanyike kwa kanda ili kuweza kupatikana muda mzuri wa kuchezeka mechi hizo,"alielezea Tibohora.

"Kwa kuwa mechi hizo zitakuwa zikiendeshwa kwa mfumo wa nyumbani na ugenini Manji ameomba klabu itakayocheza nyumbani itoe nusu ya mapato ya kwenye mechi husika iende katika mapambano hayo hapo pia klabu zitanufaika na nusu ya mapato hayo lakini pia ushindani huo utazinufaisha baadhi ya nchi."

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

KAMATI YA TUZO IMEFANYA MCHUJO KWENYE WACHEZAJI 30 WAMEBAKI 15, MKUDE, AJIBU WAMETOLEWA, ANGALIA ORODHA

Kamati ya Tuzo za Ligi Kuu ya Vodacom (VPL), iliyokutana wiki hii imeteua wachezaji 15 kwa ajili ya kuwania Tuzo ya Mchezaji Bora wa VPL msi...

TIBA YA KIIMANI

TIBA YA KIIMANI

a

a
Adbox