KOCHA wa timu ya taifa
ya Ivory Coast, Herve Renard amesema timu bora ya mashindano imetolewa
baada ya kikosi chake kuitandika Algeria na kutinga nusu fainali ya
michuano ya Mataifa ya Afrika. Mshambuliaji mpya wa Manchester City
Wilfried Bony aliifungia Ivory Coast mabao mawili katika ushindi wa
mabao 3-1 waliopata katika mchezo huo. Akihojiwa Renard amesema
anafikiri wameifunga timu bora katika mashindano. Renard amesema
walihitaji kujipanga vyema ili kujaribu kuifunga timu ambayo ni imara
kwa kitimu na mchezaji mmoja mmoja. Renard ambaye aliingoza Zambia
kushinda taji la michuano hiyo mwaka 2012, amesema wakati akiinoa
Zambia, Ivory Coast ndio ilikuwa timu bora kuliko wao lakini waliifunga
kwa changamoto ya mikwaju ya penati. Kocha huyo aliendelea kudai kuwa
kisoka na umiliki wa mpira Algeria walikuwa bora kuliko wao lakini
walitumia vyema mashabulizi yao kushtukiza wakiwategemea nyota wake Max
Gradel, Gervinho na Bony.
TANGAZA NASI: +255 655 442 255
CHANZI OPEN SCHOOL
Jumatatu, 2 Februari 2015
AFCON: RENARD ADAI WAMEING'OA TIMU BORA KATIKA MASHINDANO.
About asantemuya
Soratemplates is a blogger resources site is a provider of high quality blogger template with premium looking layout and robust design. The main mission of templatesyard is to provide the best quality blogger templates.
Jisajili kwenye:
Chapisha Maoni (Atom)
KAMATI YA TUZO IMEFANYA MCHUJO KWENYE WACHEZAJI 30 WAMEBAKI 15, MKUDE, AJIBU WAMETOLEWA, ANGALIA ORODHA
Kamati ya Tuzo za Ligi Kuu ya Vodacom (VPL), iliyokutana wiki hii imeteua wachezaji 15 kwa ajili ya kuwania Tuzo ya Mchezaji Bora wa VPL msi...
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni