STAY WITH US

LightBlog

Breaking

TANGAZA NASI: +255 655 442 255

TANGAZA NASI: +255 655 442 255

CHANZI OPEN SCHOOL

CHANZI OPEN SCHOOL

Jumatatu, 2 Februari 2015

TFF: Hatutafumbia macho imani za kishirikina kwenye soka


Mashabiki wa timu ya Yanga
Mashabiki wa timu ya Yanga
Wakati mchezo wa soka ukipiga hatua katika sayansi na teknologia katika dunia ya sasa hadi kufikia kutumia teknolojia katika kutambua kama mpira umevuka mstari wa goli au la, lakini bado dhana hiyo ni tofauti katika nchi kadha duniani na hasa barani Afrika.
Vitendo vingi zimekuwa vikishuhudiwa vikiashiria uchawi au ushirikina katika soka kitendo ambacho kinalaaniwa kwa kurudisha nyuma maendeleo ya mchezo huo maarufu duniani.
Kutokana na hilo, Shirikisho la mpira wa miguu nchini Tanzania (TFF) limesema vitendo vinavyoashiria ushirikina havitavumiliwa katika ligi kuu na timu zitaendelea kuhukumiwa kwa mujibu wa kanuni.
Mkurugenzi wa mashindano wa TFF, Boniface Wambura amesema baadhi ya timu zimeadhibiwa kwa kuamini imani za kishirikina katika jitihada za kutafuta ushindi.
“Tumeshuhudia mara kadhaa kuona mchezaji, kiongozi au shabiki akifukia kitu uwanjani au sehemu ya goli kabla ya mechi,” Wambura alisema.
“Wengine wakirusha ndege (njiwa) na baadhi ya timu zikigoma kutumia mlango wa kuingilia uwanjani au kugoma kuingia katika vyumba vya wachezaji kwa dhana potofu kuwa patakuwa na uchawi”, amesema.
Kwa mujibu wa kiongozi huyo, kanuni za ligi zinatoa adhabu ya Sh 500,000) kwa kosa au kitendo kinachoashiria uchawi au ushirikina.
Alisema kuna timu hivi karibuni iligoma kuingia chumba cha kubadilishia nguo wachezaji na ilifanikiwa kushinda mechi na toka hapo timu nyingi zimekuwa na imani hiyo.
Vitendo vya ushirikina vimekuwa vikionekana katika ligi nyingi barani Afrika na TFF iliwahi kuzihukumu timu kubwa kama vile Simba na Yanga katika miaka ya nyuma kutokana na vitendo ambavyo aidha wachezaji au mashabiki walishiriki vikiashiria ushirikina.
Lakini viongozi wengi, wakiwemo wa vilabu vya Simba na Yanga kwa wakati tofauti wamekuwa wakikana kujihusisha na vitendo hivyo wakisema ni potofu na havileti maendeleo katika mpira kwani ushindi unatokana na mazoezi.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

KAMATI YA TUZO IMEFANYA MCHUJO KWENYE WACHEZAJI 30 WAMEBAKI 15, MKUDE, AJIBU WAMETOLEWA, ANGALIA ORODHA

Kamati ya Tuzo za Ligi Kuu ya Vodacom (VPL), iliyokutana wiki hii imeteua wachezaji 15 kwa ajili ya kuwania Tuzo ya Mchezaji Bora wa VPL msi...

TIBA YA KIIMANI

TIBA YA KIIMANI

a

a
Adbox