Kiungo
wa klabu ya Juventus Federico Mattiello anayekipiga kwa mkopo katika
klabu ya Chievo amevunjika mguu baada ya kuchezewa rafu mbaya na kiungo
wa AS Roma Radja Nianggolan katika mechi ya Serie A iliyozikutanisha
timu hizo hapo jana kwenye uwanja wa San Antonio Bentegodi .
Tukio
hilo ambalo lilitokea katika dakika ya 16 ya mchezo liliteka hisia za
watu wengi walioshuhudia mchezo huo na pia lilipelekea wachezaji wa timu
zote mbili kupunguza kasi ya mchezo kwa kuhofia kuumia.
Baada
ya kiungo huyo mwenye umri wa miaka 19 kupatiwa huduma ya awali baadaye
alitolewa uwanjani katika dakika ya 19 huku mguu wake ukiwa umepinda na
nafasi yake ikachukuliwa na winga Valter Birsa
Hata
hivyo mwamuzi wa pambano hilo Paolo Silvio Mazzoleni hakumpa kadi
kiungo huyo wa Roma kwa kumvunja kinda huyo wa italia kwani walikuwa
wakigombania mpira ambao ulikuwa nusu kwa nusu (50-50).
Mechi
hiyo ilimalizika kwa sare ya 0-0 na kuifanya AS Roma kubakia katika
nafasi ya pili nyuma ya Juventus huku Chievo wakibakia nafasi ya 16
wakiwa na pointi 26 kunako ligi hiyo.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni