Simon Msuva akisindikizwa na askari kupanda usafiri wa kumuondoa
eneo la uwanja wa Taifa jana baada ya mchezo wa Ligi Kuu ya Tanzania
Bara kati ya Yanga na Simba
MCHEZAJI wa Yanga, Simon Msuva, amenusurika kupewa kichapo
kutoka kwa mashabiki wake na kuokolewa na Polisi, baada ya mchezo wa jana
kumalizika.
Msuva, aliyekuwa wa mwisho kutoka ndani ya vyumba vya
kubadilishia nguo, huku wachezaji wenzake wote wakiwaa tayari wameshaingia
ndani ya basi lao, alizongwa na mashabiki huku wakimsemea maneno makali na
kutishia kumtwanga wakidai kuwa ameuza mechi.
Winga huyo, aliokolewa na Polisi walioanza kuwatawanya
mashabiki hao kwa virungu, huku wengi wakimshika mkono Msuva na kumuweka kati
ili kumfikisha kwenye usafiri ili kuondoka eneo hilo.
Askari hao pia walionekana kuchanganyikiwa huku wakimuongoza
mchezaji huyo, kuelekea pasipojulikana huku wakitafuta basi la timu wakati
tayari walishalipita na likiwa na ukubwa ambao kamwe huwezi litafuta kama gari
ndogo.
Vurugu hizo ziliendelea huku mashabiki wakimfuata Msuva,
wakimtukana huku pia askari hao wakijitahidi kuwatawanya kwa virungu,
wakiendelea kutafuta basi la timu hadi alipofika Salum Telela na kumshika mkono
kumuelekeza basi lilipo na kuelekea katika basi akiwa chini ya ulinzi.
Baada ya Msuva kupanda basi hilo lilianza kuondoka mahala
hapo mashabiki wakilifukuza huku wakiendelea kutukana matuzi na kumtuhumu Msuva
kwa maneno kuwa ‘eti’ ameuza mechi.
Chini ya ulinzi mkali.
Wakitafuta Basi la wachezaji
Mashabiki wakimzonga Msuva
Wakirejea kupanda basi la wachezaji baada ya Telela kumfuata na kumwonyesha basi lilipo.
Wakielekea kwenye basi hilo.
Wakimpandisha basi.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni