Mabingwa wa kombe la mapinduzi Simba SC wamefanikiwa kuwagalagaza wapinzani wao wa jadi Yanga SC katika mchezo wa ligi kuu ya vodacom uliochezwa katika uwanja wa Taifa jijini Dar es salam.
Katika mchezo huo ulioshuhudia maamuzi ya utata ulianza kwa kasi ya kawaida, huku timu zote mbili zikishambuliana kwa zamu, ambapo mpaka mapumziko hakuna timu iliyokuwa imeona nyavu za wapinzani wao.
Katika dakika ya 25 Danny Mrwanda alizawadiwa kadi ya njano baada ya kumrejeshea Ramadhani Kessi baada ya Kessi kumfanyia madhambi, ambapo na Kessi nae alizawadiwa kadi ya njano.
ukio hilo lilipelekea kocha wa yanga kufanya mabadiliko ya mapema ambapo alimpumzisha Mrwanda na nafasi yake kuchukuliwa na Hussein Javu.
Katika dakika za 30 Abdi Banda alimgonga Kelvin Yondani wakati wa kona iliyokuwa inaenda kupigwa na Singano, na kupelekea mwamuzi kutoa kadi za njano kwa Banda na Yondani, kitendo kilicho amsha ghaziba kwa wachezaji wa yanga na kutaka kumvaa mwamuzi, ambapo Ngassa alifanya kazi ya ziada ya kuwatuliza wachezaji wenzao.
Katika kipindi cha pili Yanga walirejea kwa kasi, na kupelekea Simba SC kutumia mashambulizi ya kushtukiza, ambapo katika dakika ya 52 Emanuel Okwi alitumia vyemashambulizi la kushtukiza na kuipatia goli la kuongoza Simba SC.
Kuingia kwa goli hilo lilipelekea Yanga kuamisha akili zao katika kushambulia ambapo wapinzano wao Simba SC walikuwa nyuma wakizuia na kupeleka mashambulizi ya kushtukiza.
Katika dakika ya 76, Haruna Niyonzima alizawadiwa kadi nyekundu ikiwa ni baada ya kuoewa kadi ya pili ya njano wa kitendo cha kupiga mpira ambao mwamuzi alikuwa ashambuliza filimbi kuashiria madhambi.
Kutolewa kwa Haruna Niyonzima kulipelekea utawala wa mchezo kuamia kwa Simba SC, ambao walicheza kwa kuonana na kutawala mchezo, hadi mwisho wa mchezo Simba SC 1-0 yanga.
Kwa matokeo hayo yameifanya Simba SC kufikisha point 26 na kushika nafasi ya 3, huku yanga wakibakia katika uongozi wa ligi

Hakuna maoni:
Chapisha Maoni