Kocha huyo ambaye amewahi kuwa kocha msaidizi katika timu ya Azam FC, timu ya taifa ya vijana chini miaka 17 (Serengeti Boys) pamoja na ile ya wakubwa, alianza kusumbiliwa na tatizo la saratani ya koo toka mwaka jana, ambapo baada ya matibabu katika hospitali ya Muhimbili alipata nafuu na kupelekea kuendelea na shughuli zake.
Marsh alikuwa na programu maalum ya kliniki katika hospitali hiyo, na katika siku za karibuni hali yake ilirejea kuwa mbaya na leo asubuhi kukutwa na umauti.
Marsh akiwa kocha wa Kagera sugar, aliiwezesha kagera sugar kutwa kombe la Tusker ambalo lilikuwa linashikiliwa na Simba SC, na katika mchezo wa fainali aliwafunga Simba SC goli 1-0 katika uwanja wa Uhuru (uwanja wa zamani wa taifa)
Marsh akimsaidia Abdallah Kibaden katika timu ya taifa ya vijana chini ya miaka 17, alifanikisha timu hiyo kufuzu mataifa ya Afrika japo kuwa hawakushiriki kutokana na kashfa ya umri wa mchezaji Nurdin Bakari.
Vile vile Marsh akimsaidia Marcio Maximo walifanikiwa kuipeleka timu ya taifa ya wachezaji wa ndani katika michuano ya Afrika (CHAN).
Marsh ambaye ni mpenzi wa soka la vijana, kabla ya umauti alikuwa anasimamia kituo chake cha kukuza wachezaji cha Marsh Academy kilichopo Mwanza.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni