Katika mchezo huo wa ligi kuu ya vodacom Mtibwa sugar waliuwanza vyema mchezo kwa kucheza kwa uwelewano zaidi katika kipindi cha kwanza ambapo Simba SC walikuwa wakichezea mpira zaidi katika eneo lao.
Katika kipindi hicho cha kwanza ambapo Mtibwa sugar walifika langoni mwa Simba SC mara nyingi zaidi, Simba SC walikuwa wakitumia mipira mirefu, wakitaka kutumia udhaifu wa beki ya mtibwa sugar ya kutokuwa na mbio lakini kipa wa Mtibwa sugar alikuwa akiiwahi mipira yote mirefu iliyokuwa ikielekezwa kwa Okwi na Saimon Sernkuma.
Kipnid cha pili hali ilikuwa tofauti, kwani simba sc walirejea na mipango mingine tofauti na ile ya awali, mara baada ya Ramadha Singano kuingia kuchukuwa nafasi ya Sernkuma.
Kocha wa Mtibwa sugar huenda akajilaumu kwa mabadiliko aliyo yafanya ya kumpumzisha Mussa Mgosi ambate aliwapa wakati mgumu Simba SC kwa takribani dakika 75 alizocheza na nafasi yake ikachukuliwa na Vicent Barnanbas.
Mabadilok ya kumtoa Mgosi yalipelekea Simba SC kulisakama lango la Mtibwa sugar na kupelekea Mtibwa sugar kuwa na waktai mgumu katika dakika 15 za mwisho wa mchezo.
Katika dakika za nyongeza Emanuel Okwi alipiga shuti mbele ya beki Saidi Mkopi na Henry Joseph, na shuti hilo kutinga katika nyavu za Mtibwa sugar na kupaitia Simba SC pointi tatu muhimu katika mchezo huo wa leo.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni