Rais Malinzi akiwa pamoja na wajumbe wa kamati ya Utendaji ya TFF baada ya kuchaguliwa mwaka juu |
SHIRIKISHO
la Soka Tanzania (TFF) leo linafanya Mkutano Mkuu wa Mwaka mjini Morogoro kwenye
Ukumbi wa Hoteli ya Morogoro, ukiwa ni wa kwanza tangu uongozi mpya ulio chini
ya Jamal Malinzi uingie madarakani 2013.
Mkutano huu
unafanyika kwa siku mbili na unatarajiwa kuhudhuriwa na wajumbe takribani 100 kutoka
mikoa wanachama wa shirikisho hilo.
Wajumbe
watakaowakilisha mikoa ni Mwenyekiti, Katibu Mkuu na Mjumbe wa Mkutano Mkuu
kutoka kila mkoa.
Pia
kutakuwepo wawakilishi wa klabu na wajumbe wengine kutoka vyama wanachama wa TFF
ambavyo ni Chama cha Waamuzi (FRAT), Chama cha Makocha (TAFCA), Chama cha Madaktari
wa Michezo (TASMAna Chama cha Wachezaji (SPUTANZA).
Ajenda za mkutano huo ni kufungua mkutano,
uhakiki wa wajumbe, kuthibitisha ajenda, kuthibitisha muhtasari wa Mkutano Mkuu
uliopita na yatokanayo na mkutano uliopita.
Nyingine ni
hotuba ya Rais, ripoti kutoka kwa wanachama, kuthibitisha ripoti ya utekelezaji
wa Kamati ya Utendaji, kuthibitisha ripoti ya Ukaguzi wa Hesabu 2013.
Pia
kutakuwepo na agenda ya kuthibitisha ripoti ya Kamati ya Ukaguzi wa Hesabu,
kupitisha Bajeti ya 2015, marekebisho ya Katiba, mengineyo na kufunga mkutano.
Awali,
mkutano huu ulikuwa ufanyike mkoani Singida, lakini ulihamishwa kutokana na
mkoa huo kutokuwa na hoteli za kukidhi mahitaji ya wajumbe na gharama kuwa juu.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni