BAYERN Munich
imeichapa mabao 6-1 FC Porto ya Ureno katika mechi ya marudiano ya ligi ya
mabingwa ulaya iliyopigwa Allianz Arena, mjini Munich, Ujerumani.Watu wengi
walifikiri Bayern anatoka kutokana na kipigo cha 3-1 walichovuna jumatano
iliyopita, lakini walijidanganya licha ya timu hiyo kukosa baadhi ya wachezaji
nyota.
Katika mechi hiyo
ya marudiano ya robo fainali wenyeji hao walipata mabao yao kupitia kwa Thiago
Alcantara, Robert Lewandowski aliyefunga mawili, Thomas Muller, Jerome Boateng
na Xabi Alonso wakati wageni walipata bao pekee kutoka kwa Martnez.
maana yake munich wamefuzu kwa jumla ya mabao
7-4 dhidi ya wareno hao.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni