Okwi enzi hizo akiwa Etoile. |
Wakati
wewe ulifikiri Etoile du Sahel wana mpango wa kulipa zile dola 300,000
(Sh milioni 480), wenyewe walikuwa jijini Dar es Salaam wakisaidiana na
Shirikisho la Soka la Tunisia (FTF) wakitaka kumpata Emmanuel Okwi.
Makamu
wa Rais wa FTF, Krifa Jalel, amesema walimsaka Okwi bila mafanikio ili
wazungumze naye na kujua sababu ya kutoroka kazini.
Jalel
amesema waliomba waletewe Okwi bila ya mafanikio na walishirikiana na
Rais wa Etoile du Sahel (ESS), Charefeddine Ridha aliyekuwa jijini Dar
es Salaam kumpata Okwi.
Akizungumza
jijini Dar es Salaam, juzi, Jalel alisema anashangazwa na kuona Simba
wanadai fedha wakati Okwi sasa anaichezea Simba.
“Sasa
wanataka walipwe fedha za nini? Okwi si yuko hapa anaichezea Simba?
Tumetaka kukutana naye ili tuzungumze na kutatua tatizo lake, hakuna
aliyetusaidia kumpata.
“Nilizungumza
na baadhi ya viongozi wamlete, hakuna aliyetusaidia. Nilitaka kumuuliza
kwa nini aliondoka Tunisia baada ya miezi sita na hakurejea,” alisema
na alipoulizwa kama ni viongozi wa Simba ambao hawakuwapa msaada
alisisitiza:
“Wewe jua ni viongozi tena wahusika. Sasa sioni kama kuna sababu ya kulipa ingawa bado Etoile ndiyo watalitolea uamuzi.”
Alipofuatwa
kiongozi mwingine wa Etoile, yeye alisema suala la Okwi liliisha na
hawana sababu ya kulizungumzia kwa kuwa yupo Dar es Salaam walipomtoa na
anaichezea timu yake ya zamani, hivyo hakuna kilichoharibika.
“Nafikiri
unataka kunitega sijui niseme nini. Okwi yupo hapa kwenu anaichezea
timu yake. Sasa tulipe kwa kuwa anaichezea Simba! Si tayari Simba wana
mchezaji wao,” alihoji.
Etoile
iliahidi kulipa fedha hizo kwa ajili ya Okwi baada ya Simba kukubali
kumuuza ‘bure’ kupitia aliyekuwa mwenyekiti wake, Ismail Aden Rage.
Lakini
Simba imesema tayari Shirikisho la Soka la Kimataifa (Fifa), limeagiza
Simba ilipwe fedha hizo lakini Etoile wamekuwa wakisuasua na kauli
walizozitoa katika mahojiano hayo juzi, zinaonyesha huenda fedha hizo
kulipwa, itakuwa ndoto kama Simba wasiposimama kidete.
SOURCE: CHAMPIONI
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni