Na Mahamud Rajabu
Wawakilishi pekee katika michuano ya kimataifa timu ya soka ya Yanga, leo wametwaa rasmi rasmi ubingwa wa ligi kuu Tanzania bara huku wakiwa wamebaki na michezo miwili mkononi mara baada ya kuwatungua maafande wa polisi Morogoro kwa mabao 4-1, mchezo uliopigwa katika uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.
Yanga wamejikusanyia pointi 55 ambazo haziwezi kufukiwa na timu yeyote mpaka sasa.
Wakionekana kuwa na njaa ya kupata bao la mapema, Yanga walianza kwa kupeleka mashambulizi langoni mwa polisi Moro lakini shuti la Mrundi Amissi Tambe liliokolewa kwa uzuri kabisa na kipa wa Polisi Moro.
Dakika ya nane ya mchezo Yanga walifanya shambulizi lingine langoni mwa polisi Moro baada ya Msuva kuachia shuti kali ambalo hata hivyo liligonga mwamba na kurudi uwanjani na kumfikia tena Sherman ambaye alipiga nje.
Polisi Moro nao walijaribu kufanya shambulizi langoni mwa timu ya Yanga kupitia kwa Suleiman Selembe lakini shuti lake lilipaa juu.
Alikuwa ni Amissi Jocelyn Tambwe ambaye alifungua ukurasa wa mabao kwa Yanga baada ya kufunga goli dakika ya 40 kutokana na krosi maridhawa iliyopigwa na Simon Msuva.
Bao hilo lilidumu mpaka dakika 45 za kipindi cha kwanza zilimalizika na timu hizo kuelekea vumba vya kubadilishia nguo.
Yanga waliingia kwa kasi ya aina yake katika kipindi cha pili cha mchezo na kufanikiwa kuandika bao la pili kupitia kwa Amissi Tambwe ambaye aliumalizia mpira uliokuwa ukizagaa langoni mwa polisi Moro baada ya hapo awali Msuva kuachia shuti kali na kumshinda mlinda mlango wa Polisi Moro.
Polisi Moro wakionekana kutafuta walau bao moja walifanya shambulizi langoni mwa Yanga lakini Deogratius Munishi 'Dida' alikuwa makini na kuokoa mchomo huo.
Amissi Tambwe kwa mara nyingine aliiandikia Yanga bao la tatu huku akiwa amepiga hat-trick baada ya kupata krosi kutoka kwa winga mwenye kasi Mrisho Ngassa na kuutumbukiza mpira wavuni mwa Polisi Moro kwa kichwa.
Wakionekana kutakata vilivyo Yanga walishindilia msumari wa nne langoni mwa Polisi Moro mnamo dakika ya 66, safari hii akiwa ni Simon Msuva ambaye mpaka sasa ndiyo kinara wa mabao katika ligi kuu Tanzania bara likiwa ni bao lake 17 la msimu.
Polisi Moro walifanya shambulizi langoni mwa Yanga kupitia kwa Bantu Admini lakini shuti lake liliishia mikononi mwa mlinda mlango wa Yanga Deogratius Munishi 'Dida'.
Bantu Admini aliipatia Polisi Moro bao la kufutia machozi katika dakika ya 83 baada ya kuachia shuti kali kutoka nje ya 18 na kumshinda Deogratius Munishi 'Dida' ambaye alikuwa mahiri kabisa kwa siku ya leo langoni mwa timu ya Yanga.
Hii ni hat-trick ya pili kwa Tambwe ambayo imemfanya afikishe mabao 14 nyuma ya Simon Msuva mwenye mabao 17 ambaye ndiyo kinara wa wafungaji mpaka sasa.
Kwa maana hiyo sasa Hili linakuwa taji la 24 la Ligi Kuu kwa Yanga SC, baada ya awali kulitwaa katika miaka ya 1968, 1969, 1970, 1971, 1974, 1981, 1983, 1985, 1987, 1989, 1991, 1992, 1993, 1996, 1997, 1998, 2002, 2005, 2006, 2008, 2009, 2011 na 2013.
Kikosi cha Yanga SC kilikuwa; Deo Munishi ‘Dida’, Juma Abdul, Oscar Joshua, Mbuyu Twite, Kevin Yondan, Said Juma, Simon Msuva/Hussein Javu dk75, Haruna Niyonzima, Amissi Tambwe/Jerry Tegete dk75, Mrisho Ngassa na Kpah Sherman.
Polisi Moro; Abdul Ibad, Hassan Mganga, Ally Teru, Meshack Abel, Laban Kambole, Anafi Suleiman, Bantu Admin, Said Mkangu, Said Bahanuzi/Nicholas Kabipe dk51, Suleiman Kassim ‘Selembe’ na James Ambrose/Mussa Mohamed dk78.

Hakuna maoni:
Chapisha Maoni