Je, Javier Hernandez anaweza kukamilisha usajili kutoka Manchester United kwenda Real Madrid majira ya kiangazi mwaka huu?
Chicharito
amekuwa na wakati mzuri Santiago Bernabeu baada ya kujionesha kuwa yeye
ni noma akiifungia magoli muhimu Real Madrid kwenye mechi mbili.
Wiki
iliyopita Chicharito alifunga goli pekee Real Madrid wakitinga nusu
fainali ya ligi ya mabingwa ulaya (uefa Champions League) dhidi ya
Atletico Madrid na jana jumapili katika mechi ya La Liga, mshambuliaji
huyo wa Manchester United aliyepo kwa mkopo Real alikuwa kwenye kiwango
cha juu dhidi ya Celta Vigo.
Hernandez
alifunga magoli mawili katika ushindi wa 4-2 na kuamusha tena matumaini
ya Real Madrid kuipiku Barcelona kwenye mbio za ubingwa.
Katika mechi 8 alizoanza Real Madrid, sasa Chicharito amefunga magoli 6 na kutoa pasi za magoli mbili (2).
Cha
zaidi ni kwamba Chicharito ameshika nafasi ya tatu katika uwiano mzuri
kufunga magoli kwa dakika katika mechi za La Liga nyuma ya Cristiano
Ronaldo na Lionel Messi.
Kwa
mujibu wa gazeti la Hispania la AS, Javier Hernandez atawagharimu Real
Madrid euro milioni 10 sawa na paundi milioni 7 kama wataamua kumpa
usajili wa kudumu majira ya kiangazi mwaka huu.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni