Kiungo wa Chelsea Cesc Fabregas amesema kuwa kurudi kwake katika uwanja wa Emirates kulimkumbusha vitu vingi sana.
Fabregas aliandika kwenye ukurasa wake wa twitter hivi"
A day that brought back so many memories. Good game boys", akimaanisha kuwa siku ambayo ilimkumbusha vitu vingi sana wakati akiwa klabuni hapo na kumalizia kwa kuwapongeza kwa kiwango kizuri walichokionesha.
Safari hii Fabregas alirudi maskani yake hiyo ya zamani akiwa na klabu ya Chelsea huku akiwa ametinga uzi wa bluu ambapo katika mchezo huo Arsenal walilazimishwa suluhu na Chelsea.
Hata hivyo baadhi ya mashabiki wa Arsenal walionesha kuchukizwa na Fabregas na hata kufikia hatua ya kumzomea, lakini Fabregas kwa upande wake alionekana kuwa na furaha ya aina yake kurudi hapo na kuonesha ishara ya kuwapigia makofi mashabiki wote wakati akifanyiwa mabadiliko.
Kwa matokeo ya mchezo huo, Chelsea sasa wanaonekana dhahiri shahiri wanakaribia kuuchukua ubingwa huo ambao mara ya mwisho kuuchukua ilikuwa ni mwaka 2010.
Kwa upande wake Arsene Wenger, alisema kuwa timu yake ilijitahidi kuwabana vizuri chelsea huku akisema matokeo mabaya ya mwanzoni mwa msimu ndio yamewagharimu kushindwa kuendana na mbio za ubingwa.
"Ninaamini kuwa, katika kipindi cha kwanza, tulicheza kwa kiwango cha juu kabisa," Wenger aliambia tovuti ya Arsenal.

Hakuna maoni:
Chapisha Maoni