Bondia Manny Pacquiao amesafiri maili 270 kutoka Los Angeles hadi Las Vegas kwa ajili ya pambano lake dhidi ya Floyd Mayweather.
Bondia huyo raia wa Ufilipino alisafiri umbali huo ndani ya basi lake maalum akiwa pamoja na familia yake na timu yake kamili huku akiongozwa na pikipiki na magari mengine kwa ajili ya ulinzi pia.
Pambano hilo litapigwa alfajiri ya Mei 3 na Pacquiao atakuwa kambini mjini hapo pamoja na familia yake.
Kabla ya safari hiyo, kambi yake ilikuwa Los Angeles ambako amenunua jumba la kifahari.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni