Mashabiki
wa Arsenal wametoa kali ya mwaka baada ya kutaka uongozi uliondoe bango la Cesc
Fabregas kwenye Uwanja wa Emirates.
Mashabiki
hao wametaka bango la nahodha wao huyo wa zamani liondolewe kabla hajatua hapo
akiwa na Chelsea wikiendi hii.
Wamesisitiza
lazima liondolewe kwa kuwa anarejea akiwa mpinzani wao mkubwa.
Fabregas raia wa Hispania aliichezea Arsenal kwa mafanikio makubwa kabla ya kuondoka mwaka 2011 na kujiunga na Barcelona lakini akarejea England na kujiunga na Chelsea ambayo sasa inapambana na Arsenal kuwania ubingwa wa Ligi Kuu England.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni